Kashata za njugu


Mahitaji

Karanga Sukari Unga wa iliki . Maji
Namna ya kutengeneza Kaanga karanga, kisha zitoe maganda yote ziwe nyeupe. peta ili kuyatoa magamba kirahisi. Chukua sukari uchanganye na maji kidogo upike mpaka iwe nzito
Changanya unga wa iliki, kisha chukua karanga zako mimina katika sukari iliyoyeyushwa
Koroga koroga kwa mwiko mpaka ile sukari uliyoikausha ikauke Kisha mimina haraka katika sinia iliyopakwa samli kidogo na utandaze
Baadae chukua kisu ukate kate kashata zako. Zikishapoa kashata zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Comments

  1. Asante dada Muna kwa somo zuri. Nilikuwa nikitafuta kwa muda mrefu kupika kashata. Na swali. Unga wa iliki nitaupataje? Kuna unga wa kutumia badala yake? Na kuanza kupika, tunachemsha maji kwanza, au tunachanganya pembeni na kuanza kupika?

    ReplyDelete
  2. Asante sana nimekuwa nikitafua namna ya kutengeza hizi kashata kwa muda mrefu.nashukuru dada Muna Allah akubariki ila vipimo ndio vita nipige chenga haswa hayo maji ya ku changa nyanya na sukari ile kiasi chake.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu