Posts

Showing posts from July, 2011

Tambi za dengu

Image
Mahitaji Unga wa dengu ½ kilo Unga wa pilipili binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai Unga wa mchele ¼ kilo Chumvi kiasi Mafuta ya alizeti ½ lita Baking powder Namna ya kutengeneza Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga. Changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja. Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni. Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari ...

Sandwitch ya mchele

Image
Mahitaji Unga wa mchele 1/4kg Unga wa ngano 1/4kg Sukari 1/4kg Siagi 1/4kg Mayai 4 Maziwa 4 vijiko vikubwa. B.P 1 kijiko cha chai Namna ya kutengeneza Saga sukari na siagi. Tia mayai yaliyopigwa vizuri halafu tia maziwa. Nyunyiza unga wa ngano uliochungwa na mchele. Tia B.P katika vibati viwili vya sponge cake vilivyopakwa siagi Choma ukipenda paka jam baina ya katikati mbili.

Mkate wa mayai na jam

Image
Mahitaji Boflo kubwa 1 Mayai 4 Samli 1/4kg Unga wa ngano kiasi Namna ya kutengeneza Kata mkate vipande vyembamba uvipake jam, kisha vigandishe kimoja juu kingine Vunja mayai yapige sana. Kisha nyunyiza unga huku ukiendelea kupiga mayai Injika chuma cha chapatti ( frying pan) utie samli ikianza kuchemka, chovya mikate iliyogandishwa katika mchanganyiko wa mayai na ngano na ukaange ndani ya chuma, ikiwiva geuza upande wa pili Ikiwiva yaani ikiwa na rangi ya kahawia, vitoe na uvitie kwenye sahani. Tayari kwa kuliwa. Huu ni mlo kwa ajili ya watu watatu

Chatini ya karoti ,nazi na kitunguu

Image
Mahitaji Kitunguu kimoja kikubwa Karoti moja kubwa Nazi iliyokunwa nusu kikombe Pilipili mbuzi moja au mbili Kotmil fungu moja Rojo ya ukwaji nusu kikombe cha chai Chumvi kiasi Namna ya kutengeneza Kabla ya kuanza utengenezaji wakom hakikisha mbogamboga zako zinaoshwa kwa maji ya moto ili kuziweka katika hali ya usalama zaidi kiafya. Baada ya hapo, chukua karoti na vitunguu maji, katakata katika vipande vidogovidogo, kisha weka kwenye bakuli, chukua viungo vingine vyote changanya kwenye mchangayiko huo. Baada ya hapo weka kwenye mashine ya kusagia matunda, weka maji kiasi ili kurahisisha usagaji wake. Saga hadi vilainike kabisa na kuwa uji mzito, ondoa kwenye mashine na mimina kwenye bakuli tayari kwa kuliwa. Kama nilivyokueleza hapo juu, kuwa unaweza kula na chakula chochote unachopendelea kulingana na mahitaji yako. Ikiwa utapendelea kuwapa watoto, unashauriwa kutoweka pilipili wakati wa maandalizi yake. Chatini ya nazi mara nyingi hupendeza sana ikiwa italiwa ...

Make Money by Working Online

Make Money by Working Online

Mkate wa kukaanga

Image
Mahitaji Dengu zilizochemshwa - 250 gms vitunguu vya kukaanga - 25 gms hoho - 10 gms nyanya - 15 gms limao - 1 Tangawizi kijiko cha chai Kitunguu saumu kijiko kimoja cha chai masala ya mchuzi – kijiko cha chakula Chaat masala – kijiko cha chakula mkate – silesi 3 slices mafuta ya kula ½ lita Namna ya kuandaa Kata mkate katika vipande vyenye umbo unalopendelea changanya na juice ya limao na chumvi kiasi ,vikaange katika mafuta yaliyochemka . vikaange hadi view na rangi ya hudhurungi halafu viopoe. chukua sufuria kavu weka jikoni weka kijiko kimija cha mafuta kaanga vitunguu maji kisha weka tangawizi na vitunguu saumu. changanya na nyanya huku ukiendelea kukaanda hadi viive weka masala pamoja na dengu koroga hadi vichanganyike vizuri vikishachanganyika vizuri ipua chukua nyanya moja ikate silesi pamoja na vitunguu maji kata katika la mduara umbo andaa mkate wako katika sahani tayari kwa kuliwa.

Mkate wa mayai wa kukunja

Image
Mahitaji Mayai 6 Sukari vijiko3 vya chakula Unga wa ngano vijiko 3 vya chakula Maziwa ya unga vijiko 3 Vanila Foil Margarine Jam Unga wa soda ½ kijiko cha chai Namna ya kufanya Chukua bakuli kavu la plastiki au la kaure Pasua mayai yote na yamimine katika bakuli weka unga wa soda kisha yapige hadi yatike povu jeupe . Changanya na sukari huku ukiendelea kukoroga,weak maziwa ,weka unga wa ngano margarine kijiko 1 kikubwa cha chakula,vanilla matone matatu. Endelea kukoroga hadi upate uji mzito. Uache mchanganyiko huo kwa muda wa dakika tano huku ukiandaa moto kwa ajili ya kuoka mkate wako . Andaa trei lenye umbo la pembe nne kwa ajili ya kuoka mkate wako , chukua karatasi la foil na litandaze kwenye trei hiyo. Mimina mchanganyiko huo na kisha usambaze juu ya foil Oka kwa moto usio mkali sana . Baada ya kuiva toa ndani ya jiko na paka jam kwa upande wote wajuu. Baada ya hapo ikunje (roll) huku ukiondoa foil na kuiacha ilivyo. Mkate wako tayari kwa kuliwa ,unashaur...

Pudding ya mkate na siagi

Image
Mahitaji Mkate vipande vyembamba 2 au 3 Siagi 2 au3 vijiko vikubwa Zabibu 1kijiko kikubwa Maziwa 1kikombe Yai 1 Vanila kijiko kidogo kimoja Sukari 3 vijiko vikubwa Namna ya kutengeneza Paka siagi ndani ya bakuli. chukua vipande vyako viwili vya mkate, paka siagi tia zabibu katikati ya vipande hivyo kisha vibane pamoja. Weka ndani ya bakuli lako la bati Koroga yai na kulichanganya vizuri pamoja na maziwa, vanila na sukari. Mimina juu ya mkate katika bakuli . Oka polepole katika jiko na kupakua ungali umoto. Pudding yako ipo tayari kwa kuliwa, waweza kula na kinywaji chochote cha baridi.

Pudding ya chokleti

Image
Mahitaji Matunda 1(apples/berries)yachemshe Sukari 1kijiko kikubwa(castor sugar) Maziwa kidogo, Mayai madogo 2(yachemshwe) Unga vijiko vikubwa, Cocoa 1/2 kijiko kikubwa. Namna ya kutengeneza Changanya cocoa pamoja na unga au punguza unga na kutia cocoa. Pakua pamoja na custard yenye sukari nyingi kidogo.

Pudding ya tende

Image
Mahitaji Siagi/samli 1/4kg Sukari 1/4kg Mayai 2 Tende 1/2kg (iponde) Unga 1/4kg Baking powder 1tsp Namna ya kutengeneza Saga siagi na sukari mpaka ilainike Tia yai na tende Tia unga ulichanganywa na baking powder Paka samli vibati au dishi Tia pudding, funika karatasi juu, Funga uzi na tia ndani ya maji yanayochemka muda wa saa 2 na nusu, kisha epua

Crispy za mbatata

Image
Mahitaji Viazi mbatata kiasi. Chumvi kiasi. Mafuta ya kupikia ya maji. Mashine ya kuparuzia karoti (grating machine) Namna ya kupika Menya viazi vyako , kisha vioshe vizuri.Hakikisha hauuachi na majimaji Unahitaji kuwa na kile kimashine kidogo cha kuparuzia nyanya au karoti(grating machine) au kama huna waweza kutumia kisu kukatakata katika maduara membamba Vianike kidogo viwe vikavu. weka mafuta, wacha yapate moto. Vimimine ndani ya mafuta, uvikaange Geuzagauza visishikane. Wacha mpaka viwe rangi ya hudhurungi Ipua nyunyuzia chumvi , wacha vipoe. Tayari kwa kuliwa

Kaimati

Image
Mahitaji Unga wa ngano ½ kilo Sukari ¼ kilo Mafuta ya kupikia ½ lita Hamira kijiko cha chai Unga wa hiliki kijiko cha chai Namna ya kutengeneza Chukua bakuli kubwa ya plastiki weka maji vikombe viwili vya chai Weka hamira Weka unga wa hiliki Changanya na upate namna ya uji mzito sana Uache kwenye joto kwa muda hadi uumuke. Baada ya kumuka chukua mafuta weka kwenye karai la kukaangia yaweke jikoni hadi yachemke. Chukua kijiko chota uji wako na weka kwenye mafuta yaliyochemka Fanya hivyo kwa unga wote Baada ya kumalizika chukua sufuria nyingine kavu na iweke jikoni Weka maji kikombe kimojacha chai Acha yachemke weka sukari ,iache iive na ikishaanza kuwa uji unaonata weka kalimati zako huku ukizigeuzgeuza ilizikolee shira. Kaimati zako tayari kwa kuliwa waweza kunywa na chai au kinywaji chochote cha baridi.

Dengu za kukaanga

Mahitaji Dengu nzima ½ kg Mafuta ya mzeituni ¼ kikombe Unga wa kitunguu saumu kama unapendelea Hoho nyekundu 1 Hoho za njano1 Kitunguu maji Kabichi la dhambarau kiasi Unga wa Bizari nyembamba kijiko 1 Chumvi kiasi Pilipili ya unga kiasi Namna ya kutengeneza Chukua dengu zako osha na kisha chuja maji yote. Kisha weka chumvi, kitunguu saumu na unga wa binzari nzima. Katakata kabichi, kitunguu maji nah oho katika vipande vidogovidogo. Changanya hadi vichanganyike vizuri. Chukua mchanganyiko wako weka jikoni na kisha nyunyizia mafuata ya mzeituni na weka jikoni. Kaanga hadi ziive kabisa Okoa weka pembeni. Ikiwa unatumia majani ya mvuje, chukua majani ya hayo kiasi na kisha kaanga hadi yawe makavu. Na kisha weka pembeni. Baada ya hapo nyunyizia pilipili dengu zako zitakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula na vinywaji mbalimbali kama vile juisi soda n.k

Halua ya boga

Image
Mahitaji Boga ½ kilo Sukari ½ kilo Samli ½ Kilo Unga wa hiliki ½ kijiko cha chai Namna ya kutengeneza Chukua boga lako menya na kisha katakata vipande vidogo vidogo na kisha chemsha hadi viive na kuwa laini kabisa. Baada ya kuvia mwaga maji na saga mpaka uwe laini. Chukua sukari na samli na kisha changanya kwenye boga lako. Injika jikoni huku ukiendelea kusonga taratibu hadi viive vizuri. Tumia moto mdogomdogo ili kuepuka kuungua. Acha iendelee kuiva kwa muda dakika kumi na kisha ipua. Chukua sahani ya bati na ioshe na maji kisha mwaga bila kufuta. Mimina sahanini na kisha tandaza. Acha hadi ipoe. Unaweza kula na kahawa uji n.k Si hivyo unaweza kula kama ‘desert’ mara baada ya kupata mlo kamili.

Keki ya jam

Image
Maandalizi dakika 15 upishi dakika 25 Mahitaji Unga wa ngano ¼ kilo Sukari ya kawaida ¼ kilo Siagi ¼ kilo Mayai 6 Arki (Vanilla) matone matatu Baking powder kiasi Unga wa kakao kiasi ( kama utapendelea) Vya kupambia Jam ya mchanganyiko wa matunda kikombe kimoja cha chai Zabibu kavu nusu kikombe cha chai Apple moja kubwa Sukari laini (icing sugar) Namna ya kuandaa Kwenye bakuli kubwa ya udongo, weka siagi na baking powder, sukari na kisha changanya taratibu. Halafu pasua mayai yote na kisha endelea kukoroga. Baada ya hapo weka unga na changanya hadi uwe uji mzito. Chukua arki na nyunyizia kwenye mchanganyiko wako. Hii itasaidia kuifanya keki yako iwe na harufu nzuri. Ikiwa utapendelea keki yako kuwa na rangi ya brown si vibaya ukachanganya na unga wa kakao Kwenye bakuli nyingine pembeni. Chukua jam changanya na zabibu kav u. Chukua apple na menye maganda yake na katakata silesi. Kisha weka kwenye mchanganyiko wako huo. Chukua bati la kuchomea weka uji wako...

Saladi ya kuoka ya mbogamboga

Image
Mahitaji Pilipili hoho nyekundu 2 Mafuta ya parachichi au lozi (olive)vijiko 3 vya chai Mvinyo mwekundu kijiko 1 cha chai Kitunguu saumu punje 3 zilizosagwa Pilipili mbuzi moja iliyokatwakatwa Biringanya 1, lilokatwa silesi Kitunguu maji 2 vilivyokatwa silesi Nyanya 6 zilizokaushwa kwa jua Majani ya bazili kiasi Vinega kiasi Lozi nzima (olive) kiasi Namna ya kutengeneza Chukua bati la kuokea, katakata hoho katiak vipande vidogovidogo na kasha weka ndani yake. Oka kwa dakika 15 hadi zilegee. Ondoa na weka pembeni. Wakati zinapoa, changanya mafuta, kitunguu saumu na pilipili mbuzi. Weka kwenye bati la kuokea pamoja na silesi za biringanya na vitunguu weka chumvi kidogo kisha oka kwa moto wa kiasi. Acha hadi vilainike kiasi. Kwenye bakuli nyingine changanya , hoho, nyanya, lozi nzima kiasi na majani ya bazili. Kisha changanya pamoja na mbogamboga zako ulizooka. Saladi yako ipo tayari kwa kuliwa.

Makaroni ya mayonize

Image
Mahitaji Makaroni 1/2kg Mayonize 1/4kg Mafuta ya kula kijiko 1 Chumvi kiasi Maji lita 1 Figili kiasi1 Karoti 1 Tango 1 Namna ya kupika Chukua maji kiasi cha lita moja na yainjike jikoni kisha chemsha hadi yachemke kabisa. Baada ya hapo weka chumvi kiasi na kisha weka mafuta na baada ya kuchanganyika vizuri weka makaroni yako na kisha kwenye sufuria ya maji inayochemka kisha funika. Acha yachemke hadi yaive kabisa na baada ya kuhakikisha kuwa yameiva chuja maji na weka pembeni, kisha chukua bakuli weka mayonize kiasi na halafu minminia makaroni na kisha changanya vizuri hadi vichanganyike. Chukua mboga mboga zako na kisha zioshe vizuri kwa kutumia maji ya uvuguvugu, na kisha katia katia kwa mtindo utakaoupendelea kisha weka kwenye maji ya chumvi kabla ya kupamba juu ya upishi wako. Baada ya hapo chukua sahani maalum ya kuwekea salad na kisha weka macaroni yako na pamba kadri utakavyopendelea. Makaroni yako yatakuwa tayari kwa kuliwa. Chukua sahani kavu na kisha we...

Supu ya ‘Goulash’

Image
Mahitaji Nyama isiyo na mifupa ¼ kilo Tambi ¼ kilo Karoti kubwa 2 Chumvi kiasi Pilipili kiasi ikiwa unapendelea Viazi ulaya ¼ kilo Vitunguu maji 2 vikubwa Mafuta ya alisenti vijiko 3 vya mezani Ndimu 1 Namna ya kutengeneza Anza na nyama ioshe na kasha ikate vipande vidogovidogo. Kamulia ndimu na injika jikoni. Acha mpaka ive na kasha weka pembeni. Chukua viazi ulaya menya maganda na kasha vikate vipande vidovidogo, weka chumvi. Chemsha hadi viive na kasha wea pembeni. Chukua tambi zivunjevunje. Injika maji jikoni na weka chumvi kiasi pamoja na mafuta. Maji yakichemka weka tambi acha ziive na kisha chuja maji na weka pembeni. Chukua sufuria kavu na injika jikoni. Miminia mafuta na kisha kaanga vitunguu hadi view vya brown. Katakata karoti vipande vidogo vidogo na kasha weka kwenye sufuria yenye vitunguu. Kanga pamoja. Baada ya hapo weka viazi, nyama na baadaye tambi. Koroga na kasha weka chumvi kiasi na baadaye pilipili. Koroga koroga ili vichanganyike vizuri, na baadaye...

Mchuzi wa mbaazi kavu na kuku

Image
Mahitaji Vipande 4-6 vya kuku Chumvi kiasi Unga wa pilipili manga kijiko kidogo cha chai 1 Bizari kijiko 1 ½ cha mezani Juisi ya limao kijiko 1 ½ cha mezani Mbaazi mbichi ¼ kilo Kitunguu kimoja kikubwa kilichokatwa silesi Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai Unga wa karafuu ½ kijiko cha chai Mdalasini wa kijiti kimoja Pili pili mbuzi kama unatumia Bizari nyembamba kijiko 1 ½ Curry poda kijiko 1 ½ Mafuta ya alizeti robo kikombe cha chai ‘Stock’ ya kuku kiasi Nakshi baada ya upishi Hiliki iliyosagwa kijiko 1 cha chai Nyanya ndogondogo 12 Bizari nyembamba Namna ya kutengeneza Chukua nyama ya kuku na ichanganye pamoja na chumvi, limao, curru poda na unga wa pilipili. Weka kwenye bakuli na acha vikae kwa muda wa dakika 15, ili kuruhusu viungo kuingia vyema kwenye nyama hiyo. Chukua sufuria na weka jikoni, weka mafuta na anza kwa kukaanga vitunguu maji, saumu na viungo vingine.Kaanga kwa dakika 2-3 hadi vinukie kuiva.Kisha weka vipande vya kuku na kisha ...

Pudding ya mchele

Image
Mahitaji Mchele) 1/2kg(uliotwangwa) Maziwa 1 pint Sukari 1 kijiko Yai 1 Arki kiasi Njia Pasha moto maziwa katika sufuria na utie mchele uliotwangwa . Koroga mpaka uchemke Pika mpaka chenga zilainike Ondoa sufuria kwenye moto tia sukari wacha ipoe kidogo. Vunja yai liwe kiini mbali na ute mbali. Tia kiini katika mchele uliochanganywa na maziwa. Tia sukari uchanganye vizuri Piga ute utie pudding Paka sufuria samli, mimina mchagayiko choma katika oven 1/2 saa

Mkate wa ndizi

Image
Mahitaji Sukari kikombe 1 Siagi 1/3 kikombe Mayai 2 Ndizi mbivu zilizomenywa na kusagwa kikombe 1 na nusu. Maji 1/3 Unga wa ngano kikombe 1 na ½ cha chai Unga wa soda kijiko 1 cha chai Chumvi kijiko 1 cha chai Baking poda ¼ kijiko cha chai Karanga ½ kikombe cha chai Namna ya kupika Changanya sukari na siagi kwenye bakuli moja kubwa la udongo ama plastiki. Hakikisha vinachanganyika kabisa. Kisha weka mayai endelea kukoroga. Halafu unga wa ngano. Vikishalainika weka ndizi na saga kwa muda wa dakika tano. Ikiwa unatumia mashine ya kusagia sekunde 30 tu zinatosha kukamilisha zoezi hili. Chukua viungo vingine vyote vilivyobaki ispokuwa karanga na kisha weka kwenye mchanganyiko wako. Changanya vizuri hadi vichanganyike vizuri. Acha mchangayiko wako uumuke kwa muda wa dakika 30. Na baada ya hapo mimina katika bati la kuokea taya ri kwa kuoka. Oka kwa muda wa dakika 30 hadi uwe umei va kabisa . Baada ya hapo opoa na weka pembeni. Acha upoe . Ukishapoa kabisa, katakata sile...

Wali wa rangi tatu

Image
Mahitaji Kwa wali wa njano Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai Mafuta ya kupikia kijiko1 ½ Nyanya 2 zilizomenywa na kukatwakatwa Karoti 3 zilizochemshwa na kuiva Unga wa binzari 1/4 kijiko Chumvi kiasi Kwa wali wa mweupe Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai Mafuta ya kupikia kijiko1 ½ Tui la nazi kikombe 1 Unga wa hiliki Kijiko 11/2 chachai Kwa wali wa kijani Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai Mafuta ya kupikia kijiko 1 ½ Chumvi kiasi Vitunguu maji 2 Kitunguu saumu kilichopondwa 1 Tangawizi iliyopondwa 1 Nazi iliyosagwa vijiko 2 Majani 8 hadi 10 ya mnanaa Majani ya giligilani kikombe kimoja Pilipili manga kijiko 1 Garam masala kijiko 1 cha chai Namna ya kuandaa Unatakiwa kupika wali walo katika sufuria tatu tofauti. Kwa wali mweupe unatakiwa kupika kama ilivyozoeleka huku ukiongeza hiliki kama kiungo chako. Unachotakiwa kufanya ni kuosha mchele wako. Kisha injika tui jikoni weka chumvi na baadaye hiliki. Hakikisha maji uliyoinjika yana uwezo wa kuivisha w...

Juisi ya karoti

Image
Mahitaji Karoti 3 kubwa Maziwa gilasi 2.5 Sukari kiasi Maji 1gilasi yaliyochemshwa na kupozwa Arki kiasi Namna ya kutengeneza Kata caroti kama una mashine ya kusagia unaweza kuiweka kwenye mashine na kuisaga kisha weka maji, toa na ukamue maji Tia maziwa, arki juu yake koroga pamoja na sukari Onja na tayari kwa kunywewa

Kashata za njugu

Image
Mahitaji Karanga Sukari Unga wa iliki . Maji Namna ya kutengeneza Kaanga karanga, kisha zitoe maganda yote ziwe nyeupe. peta ili kuyatoa magamba kirahisi. Chukua sukari uchanganye na maji kidogo upike mpaka iwe nzito Changanya unga wa iliki, kisha chukua karanga zako mimina katika sukari iliyoyeyushwa Koroga koroga kwa mwiko mpaka ile sukari uliyoikausha ikauke Kisha mimina haraka katika sinia iliyopakwa samli kidogo na utandaze Baadae chukua kisu ukate kate kashata zako. Zikishapoa kashata zako zitakuwa tayari kwa kuliwa

Pilau ya zabibu

Image
Mahitaji Mchele kilo 1 Kuku ½ kilo Kitunguu maji 1 chenye ukubwa wa wastani Mafuta ya kupikia ¼ lita Kitunguu saumu 1 kikubwa Tangawizi mbichi 1 Mdalasini nzima vijiko 2 Iliki vijiko 2 vya mezani Uzile/ binzari nyembamba vijiko 2 vya mezani Zabibu kavu ½ kikombe cha chai. Namna ya kupika Mkate kuku au nyama na muoshe kisha mweke katika sufuria kisha weka chumvi na uchemshe mpaka awive kisha epua. Menya kitunguu maji na saumu kisha vitwange hadi vilainike. Chukua mdalasini, iliki na bizari utwange pamoja kisha uchunge unga laini saga thomu na tangawizi mbichi. Weka jikoni sufuria tia mafuta kisha anza kwa kukaanga kitunguu maji hadi kiwe na rangi ya hudhurungi kisha weka saumu kaanga kwa muda kisha tia viungo vilivyosalia. Tia vipande vya kuku halafu supu iliyosalia katika sufuria acha ichemke na vitu vyote mpaka ibaki rojo rojo. Wali ukisha upakue, utavimwagia juu ya wali ukipenda utapambia zabibu juu yake. Zabibu hizo ziloweke kwanza.

Mapishi ya tambi

Image
Futari za tambi Mahitaji Tambi ½ kg Maziwa 1/2lita Sukari kiasi Chumvi Maji 1lita Vanilla au unga wa hiliki ½ kijiko cha chai. Namna ya kupika Chukua maji na kisha weka chumvi kiasi cha nusu kijiko cha chai, injika maji jikoni na kisha yaache yachemke, weka tambi zako katika maji hayo acha zichemke kwa muda wa dakika tano. Baada ya hapo chukua hizo tambi na ziche maji yote na kisha miminia maziwa, weka sukari kiasi unachohitaji na mwisho weka vanilla au hiliki na kisha funika. Acha vichemke hadi maji yatakapoisha, pakua tayari kwa kuliwa. Tambi za kupalia Mahitaji Tambi ½ kg Maji lita 1 Chumvi kiasi Tui bubu la nazi kikombe 1 cha chai Sukari kiasi Namna ya kupika Chukua maji yaweke jikoni na kisha weka chumvi 1/2 kijiko cha chai, acha maji yachemke na kisha weka tambi acha zichemke kwa muda wa dakikia tano zitakuwa zinakaribia kuiva. Baada ya kuhakikisha kuwa zinakaribia kuiva zichuje maji yote na kisha weka tui la nazi sukari na unga wa hiliki. Acha maji yakau...

Biskuti zenye krim ya ‘custard’

Image
Mahitaji Unga wa ngano 125gm Unga wa custard 125gm Siagi 125gm Sukari 1/3 kikombe Chumvi kiasi Maziwa kikombe1 cha chai Baking powder kijiko kimoja cha chai Namna ya kutengeneza Chukua siagi yako changanya na sukari na kisha saga hadi sukari ilainike kabisa. Chunga unga wa ngano pamoja na kastadi. Weka katika mchanganyiko wako. Weka chumvi na baking powder. Chukua maziwa na miminia katika mchanganyiko wako. Kanda hadi liwe donge zito. Baada ya hapo kata madonge madogo madogo. Sukuma kama vile unataka kupika chapatti. Baada ya hapo chukua uma na chomachoma juu ya hiyo chapatti yako. Kata kata biskuti katika umbo unalopendelea na kisha weka kwenye trey iliyopakwa siagi. Oka katika moto wa kiasi Kwa muda wa dakika 15-20. Baada ya kuiva ziweke katika chombo kikavu zipoe. Krim Chukua siagi vijiko 4 vikubwa na sukari iliyosagwa “icing sugar” 100 gm na kisha changanya pamoja. Baada ya hapo chukua ladha utakayo na rangi upendayo weka kwenye mchanganyiko wako. Changany...

Kababu za muhogo

Image
Mahitaji Muhogo 1 wenye uzito wa ½ kg Kitunguu saumu kilichosagwa Chumvi kijiko kimoja Pilipili kiasi Mafuta ya kupikia lita moja Namna ya kufanya Chukua muhogo menya maganda yake na kisha ukereze kwenye mashine Baada ya upondeponde ili ulainike Weka chumvi ,kitunguu saumu na pilipili iliyosagwa. Tengeza miviringo yenye ukubwa wa ndimu Weka mafuta jikoni hadi yapate moto anza kukaanga miviringo yako hadi iwe na rangi ya njano Kababu zako ziko tayari kwa kula ,waweza kula na chatini ya nazi au ukwaju au embe .

Fagi

Image
Mahitaji Sukari 1/4 kg Siagi vijiko 3 vya chakula Maziwa ¼ kg tui ¼ kg Cocoa vijiko 3 vya chakula karanga ½ kikombe cha chai (zilizosagwa) chumvi ½ kijiko cha chai Njia Koroga cocoa kwa maji. Injika sufuria tia maziwa, cocoa, tui, na sukari. Acha mchanganyiko huo uchemke kwa muda wa dakika 30 tia chumvi katika maji ya baridi. Tia ndani ya sufuria iliyopo jikoni huku ukikoroga ili kuhahakikisha isigande wala kuungua. Iache ichemke hadi kuwa uji mzito na baada ya hapo ipua na kisha, tia karanga halafu Chukua bati, waweza hata kutumia sinia la bati, paka siagi kisha mimina uji huo na uache upoe. Baada ya kupoa katakata vipande fagi zako tayari kwa kuliwa. Ni chakula kitamu sana kwani ni mfano wa pipi lakini sio pipi halisi hivyo hupendelewa zaidi na watoto na hata wakubwa. Fagi huliwa kama vile kashata na inapendeza zaidi kama italiwa na kinywaji kisicho na sukari kama vile kahawa.

Chatini ya nazi

Image
Mahitaji Nazi iliyokunwa kikombe 1 Pilipili 3 zilizoiva Chumvi kijiko kimoja cha chai Limao au ndimu au hata ukwaju Pilipili manga za kusaga kijiko kimoja cha chai Namna ya kutengeneza Hakikisha nazi unayotumia inakuwa laini na katika hatua ya kwanza unachukua nazi yako Changanya na pilipili ambayo imesagwa Weka chumvi halafu Weka limao ,ndimu au ukwaju . Changaya pamoja na baada ya hapo weka chumvi pamoja na pilpili manga za kusaga Baada ya hapo chatne yako itkuwa tayari kwa kuliwa .

Siki ya ndimu

Image
Mahitaji Ndimu ½ kilo Sukari ½ kilo Unga wa pilipili mbuzi Chumvi kiasi Unga wa iliki ¼ kijiko Unga wa karafuu 1/8 kijiko Namna ya kutengeneza Chukua ndimu zako na osha vizuri na kisha futa maji. Kamua juisi yake na kisha weka kwenye bakuli safi na kavu. Weka chumvi kiasi. Chukua maganda yake na yakatekate vipande vyemba vyemba na kisha weka kwenye juisi yako hiyo ya limao. Baada ya hapo weka mchanganyiko wako huo juani. Anika mchanganyiko wako huo juani kwa muda wa siku sita. Tikisa chupa yako kila siku hadi maganda ya ndimu yaanze kumung’unyika. Weka sukari, unga wa pilipili na karafuu kisha changanya vizuri hadi vichanganyike kabisa. Anika juani. Fanya hivyo kila siku. Siki ikihifadhiwa vyema inaweza kudumu kwa muda wa mwaka mmoja bila kuharibika

Dagaa kamba wa kukaanga

Image
Mahitaji Dagaa kamba ½ kilo Unga wa dengu ¼ kilo Chumvi Kitunguu saumu na tangawizi iliyosagwa kijiko 1 Mafuta ya kula ½ lita Ndimu na pilipili kama unatumia Masala . Namna ya kufanya Chukua dagaa kamba wasafishe wakate vichwa na uwamenye maganda yao na kuwaacha nyama ya ndani . Waweke katika bakuli na kisha changaya na na viungo vyote tangawizi ,vitunguu saumu ,masala ndimu na pilipili chumvi. Nyunyizia unga wa dengu katika mchanganyiko huo hadi upate uji mzito . Chukua karai mimina mafuta weka jikoni na baada ya kuchemka kaanga dagaa wako hadi wawe na rangi chungwa . Fanya hivyo kwa dagaa wote katika bakuli lako na baada ya hapo kamba wako wapo tayari kwa kuliwa waweza kula wenyewe kama kitafunwa au waweza kula kama kitoweo kwa kula na chakula kingine .

Sambusa za mbogamboga

Image
Mahitaji Unga wa ngano ½ Viazi ulaya ¼kg Maji ya uvuguvugu kiasi Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 kikubwa Tangawizi kiasi Pilipili mbuzi 1 (kama unatumia) Vitunguu Maji 3 Viungo kiasi Chumvi kiasi Njegere mbichi kikombe 1 Chumvi kiasi Unga wa ngano vijiko 3 vya chakula. Namna ya kutengeza Chukua unga wa ngano ½ kg na kanda hadi ulainike kama unavyofanya kwa unga wa maandazi. Baada ya hapo chukua mbogamboga zote katakata vipande vidogovidogo na kisha waka chumvi na baadaye viungo vya unga,kisha weka jikoni. Baaada ya dakika tano ipua na weka chini. Gawa unga ukioukanda katika sehemu kumi. Tandaza kidogona kisha paka mafuta juu yake. Sukuma kama chapatti na kisha weka kwenye chuma cha kukaangia chapatti bila ya kuweka mafuta. Baada ya kubabua weka kwenye kibao cha chapati na kicha kwenye kibao halafu kata sehemu nne. Chukua unga wa ngano vijiko 3 vya mezani na kisha tengeneza uji mzito kwa ajili ya kugandisha sambusa zako. Tengeneza umbo la koni ku...

Soseji na Maharage mabichi

Image
Mahitaji Maharage meupe mabichi Nyanya moja kubwa Soseji 4 za nyama Mafuta ya alizeti kijiko 1 cha mezani Chumvi kiasi Pilipili hoho 1 Majani ya basil Yai moja Unga wa pilipili kali Namna ya kutengeneza Chukua maharage osha vizuri na chemsha hadi yaive. Baada ya hapo chukua soseji zako na katakata na kisha weka pembeni. Chukua nyanya,hoho na osha vizuri halafu katakata katika ukubwa wa kiasi. Weka katika sufuria yenye soseji. Kisha changanya na maharage. Nyunyizia mafuta na chumvi kiasi. Baada ya hapo weka jikoni na funika kwa muda wa dakika sita hadi nane. Ikiwa kama unatumia pilipili unaeza kunyunyizia kiasi kabla ya kuipua. Ipua na weka kwenye sahani. Baada ya hapo chukua chuma cha kuaangia chapatti, weka jikoni. Baada ya kupata moto weka mafuta kiasi. Chukua yai pasua. Usilikoroge ili kiini chake kionekane juu ya ute wa hilo yai. Kaanga kwa ustadi bila kugeuza na litakuwa kama jicho. Baada ya kuhakikisha kuwa limeiva. Pambia juu ya upishi wako. Chukua majani ya basil...

Ngisi wa kukaanga

Image
Mahitaji Ngisi ½ kilo Mafuta kupikia ½ lita Chumvi kiasi Juisi ya limao ama ndimu ¼ kikombe cha chai Pilipili kiasi Namna ya kutengeneza Chukua ngisi wako na kisha muoshe vizuri na toa wino wake. Unaweza kumkatakata vipande kama utapendelea. Muhifadhi katika sufuria au bakuli kavu. Baada ya hapo unaweza kumuinjika jikoni na kumwacha achemke vizuri ili kupata nyama laini. Baada ya kuiva okoa sufuria yako na weka pembeni. Kisha chukua karai la mafuta na injika jikoni. Baada ya mafuta kupata moto tosa ngisi wako na acha wachemke na mafuta hadi wabadilike rangi. Baada ya hapo ipua na weka pembeni. Chukua pilipili zako na kisha zioshe vizuri. Weka katika sufuria yenye maji kisha weka chumvi kiasi. Injika jikoni. Acha zichemke hadi ziive kabisa. Ipua na kisha saga na weka chumvi kiasi. Miminia juisi ya limao katika mchanganyiko wako. Baada ya hapo chukua ngisi wako uliokaanga na kisha kwenye bakuli weka chachandu yako. Tayari kwa kuliwa.

Saladi ya Pasta

Image
Mahitaji Fusilli pasta vikombe vitatu vya chai. (Ikiwa utapata za rangi ni vizuri zaidi) Hoho nyekundu ½ Hoho ya rangi ya njano ½ Tango ½ Nyanya 1 kubwa Mayonize (kama unapendelea) Chumvi kiasi Mafuta ya alizeti ama zaituni. Namna ya kutengeneza Chukua maji kiasi cha lita moja, injika jikoni. Kisha weka chumvi kiasi na mafuta. Acha ya chemke na baada ya hapo weka pasta kwenye maji hayo. Funika na acha ziive kabisa. Baada ya kuiva ziweke pembeni na chuja maji yote. Wakati pasta zinachemka, chukua mbogamboga osha kwa kutumia maji safi. Angalia pasta zako kama zimepoa. Changanya na mchanganyiko huo wa mbogamboga. Ikiwa unapendelea mayonize unaweza kuchangayia wakati huo, na ikiwa hupendelei unaweza kuacha hivyo hivyo. Saladi yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Kwa kiasi hiki ulichotengeneza inaweza kuliwa na watu wane.

Tambi za nyanya

Image
Mahitaji Majani ya kotmil kiasi Nyanya ya kopo ½ kikombe cha chai Chumci kiasi Unga wa pilipili manga Jibini iliyokerezwa kiasi ikiwa unapendelea. Namna ya kutengeneza Chukua nyanya zako na kisha weka kwenye sufuria ya maji. Injika jiko acha hadi maji yachemke. Ipua na mimina maji pembeni na kisha chukua nyanya zako na weka kwenye bakuli nyingine yenye maji ya baridi. Menya maganda yake na kisha katakata katika vipande vidogo vidogo. Kwenye sufuria nyingine chukua maji na kisha yaweke chumvi na kisha injika jikoni. Acha yachemke na kisha weka tambi zako. Acha hadi ziive. Baada ya kuiva ipua na chuja maji yote. Chukua sufuria nyingine na injika jikoni. Chukua mafuta na weka katika sufuria na kisha weka kitunguu saumu. Kaanga hadi kiive. Na baadaye weka nyanya ya maji. Baadaye weka unga wa pilipili manga na baadaye chumvi kiasi. Kisha weka majani ya kotmil. Punguza moto na kisha weka tambi zako na geuza geuza hadi vichanganyike kabisa. Ipua na acha wazi kwa muda wa dakika kumi....

Chauro

Mahitaji Pepeta 1/4kg Karanga 1/4kg Viazi ulaya 1/4kg Dengu 1/4kg Chumvi kijiko cha chakula Sukari kijiko cha chakula Pilipili ya unga kijiko cha chakula Mafuta ya kula lita moja Namna ya kutengeneza Menya viazi vioshe na vikatekate slesi. Weka karai la mafuta jikoni. Baada ya kuchemka weka viazi na vikaange hadi viive na kukauka. Osha karanga na kisha zikaange hadi zikauke. Osha dengu nazo zikaange. Baada ya hapo ukivitoa kwenye mafuta. Vichuje na kisha ziweke hadi zipoe. Vikishapoa vichanganye. Kisha weka kikavu na chenye nafasi. Nyunyizia sukari kiasi chumvi na pilipili. Chauro zako tayari kwa kuliwa.

Chips na silesi ya nyama

Mahitaji Viazi ulaya 1 kilo Mafuta ya kupikia lita moja Mayai 4 Nyama isiyo na mfupa silesi 4 Salad kwa ajili ya kupambia Chumvi , pilipili na ndimu kiasi Namna ya kuandaa Chukua viazi menya na katakata katika umbo la chips. Kisha kanga kwenye mafuta hadi vikauke kiasi. Chuja mafuta na kisha weka pembeni. Chukua silesi za nyama na kisha ipake chumvi na viungo vingine kama utapendelea. Unaweza kukaanga kwenye mafuta ama kuoka kwenye oven. Itakapoiva opoa na weka kwenye shani yenye chips. Vunja mayai yako na kisha kanga moja moja kwa mtindo wa jicho la ngombe na weka kwenye sahani ya chips. Gawanja chips zako katika sahani nne na kila moja weka silesi ya nyama na yai lilokaangwa. Baada ya hapo chukua saladi yako na weka pembeni ya kila sahani ya chakula chako hicho. Chips zako zipo tayari kwa kuliwa. Unaweza kula kwa kinywaji chochote unachopendelea.

Saladi ya nyama

Mahitaji Nyama ½ kilogram Mafuta 1/3 kikombe Juisi ya limao vijiko 2 Kitunguu saumu kilichopondwa vijiko 2 Chumvi ½ kijiko cha chai Pilipili manga ½ kijiko cha chai Nyanya 2 zilizoiva Karoti 1 Pilipili hoho 1 Majani ya saladi kiasi Tangawizi iliyopodwa kijiko 1 Namna ya kuandaa Anza kwa kuosha vizuri nyama. Kisha paka tangawizi, chumvi na vitunguu saumu kwenye nyama hiyo. Kisha nyunyizia unga wa pilipili manga. Ikiwa unatumia jiko la ‘oven’. Anza kwa kupaka mafuta kwenye waya wa kuchomea. Na kisha weka nyama kwenye oven. Ikiwa unatumia jiko la kawaida fanya hivyo hivyo ili kuchelea kuganda kwa nyama wakati wa kuchoma. Tandaza nyama yako vizuri kwenye waya wa kuchomea na kisha acha hadi iive. Hakikisha unaigeuzageuza ili kuepuka kuungua. Wakati nyama ikiwa jikoni, andaa saladi yako taratibu kwa kuosha vizuri na kukatakata vipande vidogo vidogo. Panga vizuri katika sahani yako tayati kwa kuliwa. Weka kwa mpangilia mbogamboga zako, hii itakusaidia kuifanya saladi yako iwe...

Nyama ya kupaka

Image
1 Mahitaji Nyama ½ kilo Mayai 4 Chumvi kiasi Samli kiasi Pilipili manga kiasi Mdaladini, iliki kiasi Bizari nzima kiasi Tangawizi iliyosagwa vijiko 2 Limao au ndimu kipande 1 Nyanya nzima za kuiva 4 kubwa Kitunguuu maji Pilipili 1 kama unapendelea Namna ya kuandaa Chukua nyama na ikatekate vipande vidogo vidogo na kisha ioshe vizuri. Injika jikoni na weka chumvi kiasi, tangawizi na juisi ya ndimu au limao. Changanya na kisha acha ichemke. Baada ya kukauka maji ya kwanza ongeza ya pili ili iive vizuri. Ikishaiva okoa na weka pembeni. Chukua sufuria nyingine kavu na injika jikoni. Weka samli na kisha anza kwa kukatia katika kitunguu maji na kisha kaanga hadi kiwe cha brown. Weka pilipili manga, iliki, mdalasini na binzari nzima na endelea kukaanga. Chukua nyanya zako na zikatekate vipande vidogo,vidogo huku ukiendelea kukoroga. Onja chumvi, ikiwa bado haijakolea vizuri, unaweza kuongeza ili iwe na ladha inayokubalika. Funika na cha viive kwa mvuke, kwa muda kam...

Supu ya samaki mchangayiko

Image
Mahitaji Minofu ya ndualo, ngizi na kamba wakubwa kilo 1 Chaza ¼ kilo Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya chakula Vitunguu maji vikubwa viwili vilivyokatwakatwa Vitungu saumu punje nne vilivyosagwa Vijiti vya figili viwili vilivyokatwakatwa vipende vidogovidogo Viazi ulaya vitatu vilivyokatwakatwa vipande vodogovidogo. Nyanya zilizomenywa na kukatwakatwa vipande vidogovidogo 1/4 kilo Nyanya ya kopo kijiko kimoja Majani ya giligilani fungu 2 Maganda ya machungwa 2 Limao au ndimu 1 Chumvi kiasi Pilipili kiasi Mvinyo mweupe kifuniko 1 cha chupa yake Namna ya kutengeneza Chukua samaki wako osha vizuri na kisha katakata vipande vidogovidogo kiasi hakikisha haviwi vidogo sana. Kwa upande wa kamba ondoa magamba yake kwanza kabla ya kuwaosha . Kisha weka pembeni kwenye bakuli safi na kavu. Kwa upande wa chaza waweke jikoni peke yake kwanza kisha chukua mvinyo miminia . maji yakiaza kupata moto , wote watajifungua. Na  ndipo uwaoshe vizuri na kisha ...