Kahawa ya baridi

Mahitaji Unga wa kahawa vijiko vine vya mezani Unga wa kakao kijiko kimoja (kama utapendelea) Maji ya moto vijiko vitano vya mezaniSukari vijiko vine vya mezani Maziwa vikombe vitatu Barafu kiasi Namna ya kutengeneza Chukua unga wa kahawa, changanya na unga wa kakao na kisha weka kwenye maji na chemsha hadi vichanganyike vizuri. Korogea sukari na acha iendelee kuchemka. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko wako wa kahawa na kisha changanya na maziwa na kisha saga kwenye mashine ya kusagia matunda. Mimina kahawa yako kwenye gilasi ndefu. Juu yake weka ice cream unayopendelea. Lakini pia kuna namna ya pili ya kutengeneza ambayo utatakiwa kuchanganya viungo vyako vyote na kuvisaga kwenye mashine. Kisha utamimina kwenye gilasi na kuweka barafu juu yake. Hapo utakuwa umemaliza kutengeneza.