Kahawa ya baridi

Mahitaji
Unga wa kahawa vijiko vine vya mezani
Unga wa
kakao kijiko kimoja (kama utapendelea)
Maji ya
moto vijiko vitano vya mezaniSukari vijiko vine vya mezani
Maziwa
vikombe vitatu
Barafu kiasi
Namna ya kutengeneza
Chukua unga wa kahawa, changanya na unga wa kakao
na kisha weka kwenye maji na chemsha hadi vichanganyike vizuri. Korogea sukari
na acha iendelee kuchemka.
Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko wako wa
kahawa na kisha changanya na maziwa na kisha saga kwenye mashine ya kusagia
matunda.
Mimina kahawa yako kwenye gilasi ndefu. Juu yake weka ice cream unayopendelea.
Lakini pia kuna namna ya pili ya kutengeneza ambayo
utatakiwa kuchanganya viungo vyako vyote na kuvisaga kwenye mashine.
Kisha utamimina kwenye gilasi na kuweka barafu juu
yake. Hapo utakuwa umemaliza kutengeneza.
Comments
Post a Comment