Wali wa dengu

Mahitaji Mchele kilo moja Kitunguu maji kimoja kilichokatwakatwa Kitunguu saumu kimoja kilichosagwa Nyama robo kilo (kama unapendelea) Dengu robo kilo Chumvi kiasi Bizari kijiko 1 Unga wa mdalasini nusu kijiko cha chai Unga wa bizari nyembamba nusu kijiko cha chai Unga wa hiliki nusu kijiko cha chai Mafuta ya kupikia
Namna ya kupika Anza kwa kuchemsha dengu zako hadi ziive kabisa. Na kisha chukua maji na injika jikoni yakichemka weka pembeni. Kwenye sufuria ya kwanza mimina mafuta ya kupikia na baada ya kupata moto weka vipande vya nyama na kanga taratibu. Weka viungo vyote ispokuwa bizari. Endelea kukaanga na vikisha chanyika vizuri miminia maji. Acha vichemke hadi viive kabisa. Baada ya maji kukauka ipua na kisha weka pembeni. Chukua sufuria nyingine na kisha weka mafuta ndani yake. Weka vitunguu saumu maji na halafu kanga hadi view vya hudhurungi. Weka mchele na endelea kukaanga. Miminia dengu zako katika mchanganyiko wako. Vikishachanganyika vizuri weka maji kiasi cha kuivisha wali. Baada ya hapo chukua nyama yako na kisha changanya na mchanganyiko wako huo. Funika na baada ya kukakamia maji, palia na mkaa juu yake. Baada ya robo saa chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu