Kuku wa kadai ( Kadai chicken)
Mahitaji
Nyama ya kuku isiyo na mifupa robo kilo
Pilipili hoho robo tatu kikombe
Kitunguu maji nusu kikombe cha chai
Nyanya
zilizokatwakatwa kikombe kimoja cha chai
Mafuta
ya kupikia kiasi
Pilipili
iliyoiva moja
Bizari
nyembamba iliyopondwa kijiko kimoja cha chai
Kitunguu
saumu na tangawizi iliyopondwa kijiko kimoja
Chumvi
kiasi
Unga
wa garam masala uliochanganywa na unga wa pilipili na unga wa kadai kijiko
kimoja cha mezani
Korosho
punje kumi
Majani
ya kotmir
Namna ya kupika
Chukua
mafuta weka jikoni na kaanga vitunguu vyote pamoja na tangawizi. Kisha weka
pilipili hoho endelea kukaanga na weka kuku. Weka viungo vyote vya unga na
koroga vizuri vichanganyike.
Endelea
kukaanga hadi aive. Baada ya hapo chukua nyanya zilizosagwa na kasha miminia
kwenye mchanganyiko wako. Vikisha chemka, chukua korosho na saga zilainike
kabisa kasha weka kwenye mchuzi wako. Weka kiasi cha maji yatakayotosha
kuivisha na kisha weka pilipili. Acha vichemke kwa muda wa dakika kumi, mchuzi
wako utakuwa tayari kwa kuliwa.
Ili
kuoneza nakshi unaweza kupamba kwa majani ya kotmir na vitunguu maji
Comments
Post a Comment