Posts

Showing posts from 2012

Wali wa dengu

Image
Mahitaji Mchele kilo moja Kitunguu maji kimoja kilichokatwakatwa Kitunguu saumu kimoja kilichosagwa Nyama robo kilo (kama unapendelea) Dengu robo kilo Chumvi kiasi Bizari kijiko 1 Unga wa mdalasini nusu kijiko cha chai Unga wa bizari nyembamba nusu kijiko cha chai Unga wa hiliki nusu kijiko cha chai Mafuta ya kupikia Namna ya kupika Anza kwa kuchemsha dengu zako hadi ziive kabisa. Na kisha chukua maji na injika jikoni yakichemka weka pembeni. Kwenye sufuria ya kwanza mimina mafuta ya kupikia na baada ya kupata moto weka vipande vya nyama na kanga taratibu. Weka viungo vyote ispokuwa bizari. Endelea kukaanga na vikisha chanyika vizuri miminia maji. Acha vichemke hadi viive kabisa. Baada ya maji kukauka ipua na kisha weka pembeni. Chukua sufuria nyingine na kisha weka mafuta ndani yake. Weka vitunguu saumu maji na halafu kanga hadi view vya hudhurungi. Weka mchele na endelea kukaanga. Miminia dengu zako katika mchanganyiko wako. Vikishachanganyika vizuri weka maji kia

Vyakula 7 vitakavyokukinga dhidi ya athari za mwanga wa jua

Image
Kwa kawaida tumekuwa tukitumia cream na vipodozi kadhaa kukinga ngozi zetu dhidi ya athari zitokanazo na mwanga wa jua. Lakini je unafahamu kuwa kuna baadhi ya vyakula vinaweza kabisa kupambana na athari hizo bila msaada wa vipodozi. Kutokana na kutambua vizuri vyakula hivyo, nimeona si nikuletee ili upate kuelewa na ikibidi kutumia. Vyakula hivyo ni: Samaki wa maji baridi Matunda yenye rangi nyekundu na mboga za majani Mboga mboga za majani zenye rangi ya kijani iliyokolea Mafuta ya Lozi 'Olive Oil' Matunda yenye Vitamin C kwa wingi Chai ya kijani Choklet