Posts

Showing posts from October, 2016

Salad ya kitunguu maji

Image
Mahitaji Vitunguu maji kiasi unachohitaji Chumvi Vinegar/ Limao/Ndimu Namna ya kutengeneza Chukua vitunguu na vikate vyembambavyemba, na kisha weka maji na kisha chumvi kidogo kwenye bakuli. Baada ya hapo visugue kidogo ili kuondoa ukali. Baada ya hapo kamulia ndimu. Ikiwa una vinegar unaweza kutumia badala ya ndimu ama limao. Ili kuongeza nakshi pia si vibaya ukakatia nyanya, tango, pilipili na hata majani ya kotmir. Salad yako ipo tayari kwa kuliwa.

Kuku wa kadai ( Kadai chicken)

Image
Mahitaji Nyama ya kuku isiyo na mifupa robo kilo Pilipili hoho robo tatu kikombe Kitunguu maji nusu kikombe cha chai Nyanya zilizokatwakatwa kikombe kimoja cha chai Mafuta ya kupikia kiasi Pilipili iliyoiva moja Bizari nyembamba iliyopondwa kijiko kimoja cha chai Kitunguu saumu na tangawizi iliyopondwa kijiko kimoja Chumvi kiasi Unga wa garam masala uliochanganywa na unga wa pilipili na unga wa kadai kijiko kimoja cha mezani Korosho punje kumi Majani ya kotmir Namna ya kupika Chukua mafuta weka jikoni na kaanga vitunguu vyote pamoja na tangawizi. Kisha weka pilipili hoho endelea kukaanga na weka kuku. Weka viungo vyote vya unga na koroga vizuri vichanganyike. Endelea kukaanga hadi aive. Baada ya hapo chukua nyanya zilizosagwa na kasha miminia kwenye mchanganyiko wako. Vikisha chemka, chukua korosho na saga zilainike kabisa kasha weka kwenye mchuzi wako. Weka kiasi cha maji yatakayotosha kuivisha na kisha weka pilipili. Acha vichemke kwa muda wa dakik