Salad ya kitunguu maji


Mahitaji
Vitunguu maji kiasi unachohitaji
Chumvi
Vinegar/ Limao/Ndimu
Namna ya kutengeneza
Chukua vitunguu na vikate vyembambavyemba, na kisha weka maji na kisha chumvi kidogo kwenye bakuli. Baada ya hapo visugue kidogo ili kuondoa ukali. Baada ya hapo kamulia ndimu. Ikiwa una vinegar unaweza kutumia badala ya ndimu ama limao.
Ili kuongeza nakshi pia si vibaya ukakatia nyanya, tango, pilipili na hata majani ya kotmir.
Salad yako ipo tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu