Posts

Showing posts from January, 2016

Keki ya Pundamilia

Image
Mahitaji Sukari kikombe kimoja cha chai Mayai manne Maziwa kikombe kimoja cha chai Mafuta ya kupikia kikombe kimoja cha chai Unga wa ngano vikombe viwili vya chai Vanila matone matatu au unga wa hiliki nusu kijiko cha chai Unga wa kokoa nyeusi vijiko viwili vya chai Baking powder kijiko kimoja cha chai . Namna ya kuandaa Chukua sukari na weka kwenye bakuli lenye nafasi lenye uwezo wa kuchukua kiasi cha kilo moja na nusu hadi kilo mbili. Weka sukari na mayai na koroga hadi vichanganyike kabisa. Kama una mashine ya mkono ya kusagia unaweza kutumia. Weka maziwa na mafuta na endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri Katika bakuli jIngine changanya baking powder, unga wa hiliki au vanilla pamoja na unga wa ngano. Weka huo unga kwenye mchanganyiko wako wa mayai na sukari kasha endelea kuchanganya. Gawa mchanganyiko sehemu mbili sawa Sehemu moja iweke pembeni na nyingine weka unga wa kakao na endelea kukoroga na uichanganye vizuri.. Mimina kwenye trey au s