Keki ya Pundamilia

Mahitaji
Sukari kikombe kimoja cha chai
Mayai manne
Maziwa kikombe kimoja cha chai
Mafuta ya kupikia kikombe kimoja cha chai
Unga wa ngano vikombe viwili vya chai
Vanila matone matatu au unga wa hiliki nusu kijiko cha chai
Unga wa kokoa nyeusi vijiko viwili vya chai
Baking powder kijiko kimoja cha chai

.


Namna ya kuandaa

Chukua sukari na weka kwenye bakuli lenye nafasi lenye uwezo wa kuchukua kiasi cha kilo moja na nusu hadi kilo mbili. Weka sukari na mayai na koroga hadi vichanganyike kabisa. Kama una mashine ya mkono ya kusagia unaweza kutumia.
Weka maziwa na mafuta na endelea kuchanganya hadi vichanganyike vizuri
Katika bakuli jIngine changanya baking powder, unga wa hiliki au vanilla pamoja na unga wa ngano.
Weka huo unga kwenye mchanganyiko wako wa mayai na sukari kasha endelea kuchanganya.
Gawa mchanganyiko sehemu mbili sawa
Sehemu moja iweke pembeni na nyingine weka unga wa kakao na endelea kukoroga na uichanganye vizuri..
Mimina kwenye trey au sufuria ya kuokea vijiko vitatu vya mchanganyiko usiokuwa na kakao, kisha weka wenye kakao. Fanya hiyo hadi mchanganyiko wako umalizike. (usisubiri mchanganyiko usambae).
Oka kwa moto wa kiasi hadi itakapoiva kabisa. Ipua na weka pembeni. Keki yako ipo tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu