Tambi za nyanya

Mahitaji
Majani ya kotmil kiasi
Nyanya ya kopo ½ kikombe cha chai
Chumci kiasi
Unga wa pilipili manga
Jibini iliyokerezwa kiasi ikiwa unapendelea.
Namna ya kutengeneza
Chukua nyanya zako na kisha weka kwenye sufuria ya maji. Injika jiko acha hadi maji yachemke. Ipua na mimina maji pembeni na kisha chukua nyanya zako na weka kwenye bakuli nyingine yenye maji ya baridi. Menya maganda yake na kisha katakata katika vipande vidogo vidogo.
Kwenye sufuria nyingine chukua maji na kisha yaweke chumvi na kisha injika jikoni. Acha yachemke na kisha weka tambi zako. Acha hadi ziive. Baada ya kuiva ipua na chuja maji yote.
Chukua sufuria nyingine na injika jikoni. Chukua mafuta na weka katika sufuria na kisha weka kitunguu saumu. Kaanga hadi kiive. Na baadaye weka nyanya ya maji. Baadaye weka unga wa pilipili manga na baadaye chumvi kiasi. Kisha weka majani ya kotmil.
Punguza moto na kisha weka tambi zako na geuza geuza hadi vichanganyike kabisa. Ipua na acha wazi kwa muda wa dakika kumi.
Mpaka hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa. Unaweza kula kama chakula cha mchana ama usiku na kujisikia vizuri.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za dengu