Saladi ya Pasta

Mahitaji
Fusilli pasta vikombe vitatu vya chai. (Ikiwa utapata za rangi ni vizuri zaidi)
Hoho nyekundu ½
Hoho ya rangi ya njano ½
Tango ½
Nyanya 1 kubwa
Mayonize (kama unapendelea)
Chumvi kiasi
Mafuta ya alizeti ama zaituni.
Namna ya kutengeneza

Chukua maji kiasi cha lita moja, injika jikoni. Kisha weka chumvi kiasi na mafuta. Acha ya chemke na baada ya hapo weka pasta kwenye maji hayo. Funika na acha ziive kabisa. Baada ya kuiva ziweke pembeni na chuja maji yote.
Wakati pasta zinachemka, chukua mbogamboga osha kwa kutumia maji safi. Angalia pasta zako kama zimepoa. Changanya na mchanganyiko huo wa mbogamboga.
Ikiwa unapendelea mayonize unaweza kuchangayia wakati huo, na ikiwa hupendelei unaweza kuacha hivyo hivyo.
Saladi yako itakuwa tayari kwa kuliwa. Kwa kiasi hiki ulichotengeneza inaweza kuliwa na watu wane.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu