Soseji na Maharage mabichi


Mahitaji
Maharage meupe mabichi
Nyanya moja kubwa
Soseji 4 za nyama
Mafuta ya alizeti kijiko 1 cha mezani
Chumvi kiasi
Pilipili hoho 1
Majani ya basil
Yai moja
Unga wa pilipili kali
Namna ya kutengeneza
Chukua maharage osha vizuri na chemsha hadi yaive. Baada ya hapo chukua soseji zako na katakata na kisha weka pembeni.
Chukua nyanya,hoho na osha vizuri halafu katakata katika ukubwa wa kiasi. Weka katika sufuria yenye soseji. Kisha changanya na maharage. Nyunyizia mafuta na chumvi kiasi. Baada ya hapo weka jikoni na funika kwa muda wa dakika sita hadi nane. Ikiwa kama unatumia pilipili unaeza kunyunyizia kiasi kabla ya kuipua. Ipua na weka kwenye sahani.
Baada ya hapo chukua chuma cha kuaangia chapatti, weka jikoni. Baada ya kupata moto weka mafuta kiasi. Chukua yai pasua. Usilikoroge ili kiini chake kionekane juu ya ute wa hilo yai. Kaanga kwa ustadi bila kugeuza na litakuwa kama jicho. Baada ya kuhakikisha kuwa limeiva. Pambia juu ya upishi wako.
Chukua majani ya basil na kisha, osha katika maji ya moto na katia katika juu ya upishi wako ili kuweka nakshi.
Hadi hapo chakula chako kitakuwa tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu