Makaroni ya mayonize

Mahitaji

Makaroni 1/2kg
Mayonize 1/4kg
Mafuta ya kula kijiko 1
Chumvi kiasi
Maji lita 1
Figili kiasi1
Karoti 1
Tango 1


Namna ya kupika

Chukua maji kiasi cha lita moja na yainjike jikoni kisha chemsha hadi yachemke kabisa. Baada ya hapo weka chumvi kiasi na kisha weka mafuta na baada ya kuchanganyika vizuri weka makaroni yako na kisha kwenye sufuria ya maji inayochemka kisha funika.

Acha yachemke hadi yaive kabisa na baada ya kuhakikisha kuwa yameiva chuja maji na weka pembeni, kisha chukua bakuli weka mayonize kiasi na halafu minminia makaroni na kisha changanya vizuri hadi vichanganyike.

Chukua mboga mboga zako na kisha zioshe vizuri kwa kutumia maji ya uvuguvugu, na kisha katia katia kwa mtindo utakaoupendelea kisha weka kwenye maji ya chumvi kabla ya kupamba juu ya upishi wako.

Baada ya hapo chukua sahani maalum ya kuwekea salad na kisha weka macaroni yako na pamba kadri utakavyopendelea. Makaroni yako yatakuwa tayari kwa kuliwa.

Chukua sahani kavu na kisha weka makaroni yako tayari kwa kuliwa,chakula hiki hutumiwa kama chakula maalum kwa watu maalum.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu