Biskuti zenye krim ya ‘custard’


Mahitaji
Unga wa ngano 125gm
Unga wa custard 125gm
Siagi 125gm
Sukari 1/3 kikombe
Chumvi kiasi
Maziwa kikombe1 cha chai
Baking powder kijiko kimoja cha chai

Namna ya kutengeneza

Chukua siagi yako changanya na sukari na kisha saga hadi sukari ilainike kabisa. Chunga unga wa ngano pamoja na kastadi. Weka katika mchanganyiko wako. Weka chumvi na baking powder. Chukua maziwa na miminia katika mchanganyiko wako. Kanda hadi liwe donge zito.
Baada ya hapo kata madonge madogo madogo. Sukuma kama vile unataka kupika chapatti. Baada ya hapo chukua uma na chomachoma juu ya hiyo chapatti yako.
Kata kata biskuti katika umbo unalopendelea na kisha weka kwenye trey iliyopakwa siagi. Oka katika moto wa kiasi
Kwa muda wa dakika 15-20. Baada ya kuiva ziweke katika chombo kikavu zipoe.

Krim Chukua siagi vijiko 4 vikubwa na sukari iliyosagwa “icing sugar” 100 gm na kisha changanya pamoja. Baada ya hapo chukua ladha utakayo na rangi upendayo weka kwenye mchanganyiko wako. Changanya hadi ichangayike vizuri.
Baada ya hapo chukua krim yako na chota kwenye kijiko na weka kwenye biskuti moja kisha gandishia nyingine juu yake. Fanya hivyo kwa biskuti zote. Acha zigande na baada ya hapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu