Siki ya ndimu

Mahitaji
Ndimu ½ kilo
Sukari ½ kilo
Unga wa pilipili mbuzi
Chumvi kiasi
Unga wa iliki ¼ kijiko
Unga wa karafuu 1/8 kijiko
Namna ya kutengeneza
Chukua ndimu zako na osha vizuri na kisha futa maji. Kamua juisi yake na kisha weka kwenye bakuli safi na kavu. Weka chumvi kiasi.
Chukua maganda yake na yakatekate vipande vyemba vyemba na kisha weka kwenye juisi yako hiyo ya limao. Baada ya hapo weka mchanganyiko wako huo juani.
Anika mchanganyiko wako huo juani kwa muda wa siku sita. Tikisa chupa yako kila siku hadi maganda ya ndimu yaanze kumung’unyika.
Weka sukari, unga wa pilipili na karafuu kisha changanya vizuri hadi vichanganyike kabisa. Anika juani. Fanya hivyo kila siku.
Siki ikihifadhiwa vyema inaweza kudumu kwa muda wa mwaka mmoja bila kuharibika

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu