Ngisi wa kukaanga

Mahitaji
Ngisi ½ kilo
Mafuta kupikia ½ lita
Chumvi kiasi
Juisi ya limao ama ndimu ¼ kikombe cha chai
Pilipili kiasi
Namna ya kutengeneza
Chukua ngisi wako na kisha muoshe vizuri na toa wino wake. Unaweza kumkatakata vipande kama utapendelea.
Muhifadhi katika sufuria au bakuli kavu.
Baada ya hapo unaweza kumuinjika jikoni na kumwacha achemke vizuri ili kupata nyama laini. Baada ya kuiva okoa sufuria yako na weka pembeni.
Kisha chukua karai la mafuta na injika jikoni. Baada ya mafuta kupata moto tosa ngisi wako na acha wachemke na mafuta hadi wabadilike rangi.
Baada ya hapo ipua na weka pembeni.
Chukua pilipili zako na kisha zioshe vizuri. Weka katika sufuria yenye maji kisha weka chumvi kiasi. Injika jikoni. Acha zichemke hadi ziive kabisa.
Ipua na kisha saga na weka chumvi kiasi. Miminia juisi ya limao katika mchanganyiko wako.
Baada ya hapo chukua ngisi wako uliokaanga na kisha kwenye bakuli weka chachandu yako. Tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu