Mchuzi wa mbaazi kavu na kuku


Mahitaji
Vipande 4-6 vya kuku
Chumvi kiasi
Unga wa pilipili manga kijiko kidogo cha chai 1
Bizari kijiko 1 ½ cha mezani
Juisi ya limao kijiko 1 ½ cha mezani
Mbaazi mbichi ¼ kilo
Kitunguu kimoja kikubwa kilichokatwa silesi
Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 cha chai
Unga wa karafuu ½ kijiko cha chai
Mdalasini wa kijiti kimoja
Pili pili mbuzi kama unatumia
Bizari nyembamba kijiko 1 ½
Curry poda kijiko 1 ½
Mafuta ya alizeti robo kikombe cha chai
‘Stock’ ya kuku kiasi

Nakshi baada ya upishi

Hiliki iliyosagwa kijiko 1 cha chai
Nyanya ndogondogo 12
Bizari nyembamba


Namna ya kutengeneza

Chukua nyama ya kuku na ichanganye pamoja na chumvi, limao, curru poda na unga wa pilipili. Weka kwenye bakuli na acha vikae kwa muda wa dakika 15, ili kuruhusu viungo kuingia vyema kwenye nyama hiyo.

Chukua sufuria na weka jikoni, weka mafuta na anza kwa kukaanga vitunguu maji, saumu na viungo vingine.Kaanga kwa dakika 2-3 hadi vinukie kuiva.Kisha weka vipande vya kuku na kisha kanga hadi view na rangi ya hudhurungi. Baada ya hapo opoa vipande hivyona weka pembeni. Kisha weka mbaazi kwenye sufuria uliotoa vipande vya nyama ya kuku.
Kisha weka bizari mchanganyiko wa vitunguu, stock ya kuku. Kanga na weka maji kiasi. Funika kwa dakika 20 au hadi utakapo hakikisha zimeiva. Rudisha tena nyama ya kuku. Acha vichemke pamoja hadi vifanye mbaazi ziwe na rojo. Ipua na weka pembeni.

Kwenye kisufuria kingine kidogo Kaanga nyanya zako kwenye mafuta kiasi, hadi maganda yake yaanze kupasuka. Changanya na viungo vingine vilivyobaki na kisha miminia kwenye mchanganyiko wa kuku na mbaazi. Chukua unga wa hilki na nyunyizia juu yake.

Mchuzi wako uko tayari kwa kuliwa. Unaweza kula na wali ama ugali.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu