Kababu za muhogo

Mahitaji
Muhogo 1 wenye uzito wa ½ kg
Kitunguu saumu kilichosagwa
Chumvi kijiko kimoja
Pilipili kiasi

Mafuta ya kupikia lita moja

Namna ya kufanya
Chukua muhogo menya maganda yake na kisha ukereze kwenye mashine
Baada ya upondeponde ili ulainike
Weka chumvi ,kitunguu saumu na pilipili iliyosagwa.
Tengeza miviringo yenye ukubwa wa ndimu
Weka mafuta jikoni hadi yapate moto anza kukaanga miviringo yako hadi iwe na rangi ya njano
Kababu zako ziko tayari kwa kula ,waweza kula na chatini ya nazi au ukwaju au embe .

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu