Dengu za kukaanga

Mahitaji
Dengu nzima ½ kg
Mafuta ya mzeituni ¼ kikombe
Unga wa kitunguu saumu kama unapendelea
Hoho nyekundu 1
Hoho za njano1
Kitunguu maji
Kabichi la dhambarau kiasi
Unga wa Bizari nyembamba kijiko 1
Chumvi kiasi
Pilipili ya unga kiasi
Namna ya kutengeneza
Chukua dengu zako osha na kisha chuja maji yote. Kisha weka chumvi, kitunguu saumu na unga wa binzari nzima. Katakata kabichi, kitunguu maji nah oho katika vipande vidogovidogo. Changanya hadi vichanganyike vizuri.
Chukua mchanganyiko wako weka jikoni na kisha nyunyizia mafuata ya mzeituni na weka jikoni.
Kaanga hadi ziive kabisa Okoa weka pembeni.
Ikiwa unatumia majani ya mvuje, chukua majani ya hayo kiasi na kisha kaanga hadi yawe makavu. Na kisha weka pembeni.
Baada ya hapo nyunyizia pilipili dengu zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Unaweza kula na vinywaji mbalimbali kama vile juisi soda n.k

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu