Posts

Showing posts from May, 2017

Munna coloured cookies

Image
Mahitaji Unga wa ngano 1kg  Siagi 1/2 Sukari 1/2 Vanilla kiasi Baking powder Namna ya kutengeneza Chukua samli na unga changanya kisha weka baking poda. Changanya vizuri kisha weka maji kidogo kidogo kupata donge gumu. Gawanya donge lako katika sehemu Tatu.  Moja utaliacha lilivyo na mengine utaweka ranging unayopendelea kila moja. Mimi nilipenda kijani na nyekundu. Sukuma na kata katika viduara kidogo kisha oka kwa moto wa wastani hakikisha haviuungui.

Tambi za Nazi na vanilla

Image
Mahitaji Tambi 1/2kg Chumvi kiasi Sukari kiasi Tui bubu la Nazi, nusu kikombe cha chai Vanilla  Maji Lita moja Namna ya kutengeneza   Chukua maji Lita moja na injika jikoni weka na chumvi kiasi. Acha yachemke na kisha vunja tambi zako na tosa kwenye maji hayo. Acha zichemke hadi zianze kuiva. Chuja maji kwenye tambi hizo na kisha mimina like tui bubu. Kisha weka sukari na baadaye matone matatu ya vannila. Acha zichemke ili maji yakakamie. Pakua kwenye sahani tayari kwa kuliwa. Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani unaweza kula kama futari.

Visheti vya kilua

Image
Mahitaji  Unga wa ngano 1kg Sukari 1/4 kg Nazi iliyokunwa kikombe 1 cha chai Samli 1/4 kg Vanilla matone matatu Icing Sugar 1/2kg Mafuta ya kula 1/2 Lita Baking powder kijiko 1 cha chai Maji vikombe 2 vya chai Namna ya kutengeneza  Changanya samli na Nazi . Baada ya hapo weka baking powder endelea kuchanganya na kisha weka unga na vanilla. Changanya hadi vichanganuike vizuri. Weka maji kidogo kidogo hadi update donge gumu. Kata matonge Mdogo Mdogo tayari kwa kusukuma. Sukuma taratibu na kisha kata mkato wa kashata Baada ya hapo kuñja kwa kukutanisha na kubinua pembe ili upate umbo la kilua. Ukimaliza injika karai la mafuta jikoni na anza kukaanga. Hakikisha haviwi brown sana lakini vinaiva na kukauka.Chukua icing sugar weka kwenye bakuli pana na kisha baada ya kuopoa visheti vyako chuja mafuta na weka kwenye bakuli hilo lenye sukari. Peta ili kuruhususukari ichanganyike vizuri. Hakikisha unafanya hivyo vikiwa bado vya moto.Fanya hivyo kwa vipande vyote. India k

Ubuyu mweupe wa sukari

Image
Ubuyu mweupe wa vanilla unaofahamika kama munna Ubuyu. Huu ni ubuyu mtamu unaweza kuliwa na wanawake na wanaume pia, wakubwa kwa watoto.Pamoja na Sifa hiyo, aina hii ya ubuyu ndio hasa inayopendwa na wanaume wengine.   Mahitaji Ubuyu kopo moja la Lita Tano  Sukari kg 3 Vanilla Unga wa ubuyu kg 1  Maji gilasi 3   Namba ya kutengeneza Chukua sukari changanya na maji kisha injika jikoni. Acha sukari ichemke na iive . kisha ipua na weka chini. Weka vanilla matone machache. Mimina ubuyu kwenye sufuria yenye shira na endelea kukoroga. Fanya hivyo hadi uchanganyike vizuri. Anza kuweka unga wa ubuyu hadi ubuyu wako ujishike vizuri. Ukishajishika chukua ubuyu wako weka kwenye beseni na funika na kitambaa cha jinja.Acha hadi upoe. Na hapo utakuwa tayari kwa kulipa.