Ubuyu mweupe wa sukari

Ubuyu mweupe wa vanilla unaofahamika kama munna Ubuyu. Huu ni ubuyu mtamu unaweza kuliwa na wanawake na wanaume pia, wakubwa kwa watoto.Pamoja na Sifa hiyo, aina hii ya ubuyu ndio hasa inayopendwa na wanaume wengine.
 Mahitaji

Ubuyu kopo moja la Lita Tano
 Sukari kg 3
Vanilla Unga wa ubuyu kg 1
 Maji gilasi 3

 Namba ya kutengeneza

Chukua sukari changanya na maji kisha injika jikoni. Acha sukari ichemke na iive . kisha ipua na weka chini. Weka vanilla matone machache. Mimina ubuyu kwenye sufuria yenye shira na endelea kukoroga. Fanya hivyo hadi uchanganyike vizuri. Anza kuweka unga wa ubuyu hadi ubuyu wako ujishike vizuri. Ukishajishika chukua ubuyu wako weka kwenye beseni na funika na kitambaa cha jinja.Acha hadi upoe. Na hapo utakuwa tayari kwa kulipa.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu