Posts

Showing posts from June, 2016

Kahawa ya baridi

Image
Mahitaji   Unga wa kahawa vijiko vine vya mezani   Unga wa kakao kijiko kimoja (kama utapendelea)   Maji ya moto vijiko vitano vya mezaniSukari vijiko vine vya mezani   Maziwa vikombe vitatu   Barafu kiasi Namna ya kutengeneza Chukua unga wa kahawa, changanya na unga wa kakao na kisha weka kwenye maji na chemsha hadi vichanganyike vizuri. Korogea sukari na acha iendelee kuchemka. Chukua vijiko viwili vya mchanganyiko wako wa kahawa na kisha changanya na maziwa na kisha saga kwenye mashine ya kusagia matunda. Mimina kahawa yako kwenye gilasi ndefu.   Juu yake weka ice cream unayopendelea. Lakini pia kuna namna ya pili ya kutengeneza ambayo utatakiwa kuchanganya viungo vyako vyote na kuvisaga kwenye mashine. Kisha utamimina kwenye gilasi na kuweka barafu juu yake. Hapo utakuwa umemaliza kutengeneza.

Wali wa kuaanga

Image
Mahitaji Kiporo cha wali wa Jasmine vikombe viwili vya chai Majani ya kitunguu maji   matatu hadi manne yaliyokatwa katwa Punje 3 -4 za kitunguu saumu kilichopondwa Sosi ya soya vijiko viwili vya chai Sosi ya samaki nusu kijiko cha chai Nyama ya samaki aina ya kaa Yai moja Sukari nusu kijiko Mafuta ya alizeti kiasi Vya kupambia Kipande kimoja cha ndimu Tango silesi mbili au tatu Sosi ya samaki, Pilipili ndefu na limao Namna ya kupika Chukua chuma cha kukaangia chapatti na weka mafuta kiasi na kisha weka vitunguu saumu na kanga hadi viwe vya hudhurungi. Kisha weka yai na endelea kukaanga hadi liive.   Weka nyama ya kaa na endelea kukaanga. Baada ya hapo miminia   wali na endelea kukaanga huku ukiuchanganya vizuri. Miminia sosi ya soya na halafu ya samaki kabla ya kunyunyizia sukari. Endelea kukaanga hadi viive vizuri kisha miminia majani ya vitunguu yaliyokatwa katwa. Hakikisha yanachanganyika vizuri na wali wako kabla ya kuumimina kwenye sahani. P