Wali wa kuaanga
Kiporo cha wali wa Jasmine vikombe viwili vya chai
Majani ya kitunguu maji matatu hadi manne yaliyokatwa katwa
Punje 3 -4 za kitunguu saumu kilichopondwa
Sosi ya soya vijiko viwili vya chai
Sosi ya samaki nusu kijiko cha chai
Nyama ya samaki aina ya kaa
Yai moja
Sukari nusu kijiko
Mafuta ya alizeti kiasi
Vya
kupambia
Kipande kimoja cha ndimu
Tango silesi mbili au tatu
Sosi ya samaki, Pilipili ndefu na limao
Namna
ya kupika
Chukua chuma cha kukaangia chapatti na weka mafuta
kiasi na kisha weka vitunguu saumu na kanga hadi viwe vya hudhurungi. Kisha
weka yai na endelea kukaanga hadi liive.
Weka nyama ya kaa na endelea kukaanga. Baada ya hapo miminia wali na endelea kukaanga huku ukiuchanganya
vizuri. Miminia sosi ya soya na halafu ya samaki kabla ya kunyunyizia sukari.
Endelea kukaanga hadi viive vizuri kisha miminia majani ya vitunguu yaliyokatwa
katwa. Hakikisha yanachanganyika vizuri na wali wako kabla ya kuumimina kwenye
sahani.
Pamba wali wako kwa viungo vilivyo pembeni. Kwanza
chukua ndimu na kata kipande kisha weka kwenye sahani ya wali. Kisha chukua
tango na katakata kwa mtindo utakaopendelea ili kuleta nakshi katika chakula
chako. Tengeneza sosi ya kulia chakula chako kwa kuchanganya sosi ya samaki,
pilipili na limao.
Ukitaka kula hakikisha unatumia sosi hii , kama
mchuzi wake ili kuongeza ladha zaidi katika wali wako.
Chakula hiki kinaweza kuliwa mchana au hata usiku
na kumfanya mlaji afurahie ladha yake.
Comments
Post a Comment