Posts

Showing posts from August, 2011

Mkate wa mbogamboga

Image
Mahitaji Mbogamboga za kujazia Vitunguu vitatu vilivyokatwakatwa Nyanya 2 zilizokatwakatwa Hoho 1 ilikatwakatwa kitunguu saumu kilichopondwa kijiko 1 cha mezani Tangawizi iliyosagwa kijiko 1 cha mezani Unga wa bizari nzima kijiko 1 cha chai Sukari kijiko 1 cha chai Kotmiri fungu 1 Mafuta ya kupikia kiasi Chumvi kiasi Kwa mkate unga wa ngano vikombe 3 vya chai Hamiara kijiko 1 cha chakula Suakri kijiko 1 cha chakula Chumvi kijiko 1 cha chai Mafuta ya kula vijiko 2 Jibini kiasi Namna ya kuandaa Vya kujazia Chukua mafuta na weka kwenye sufuria kisha ijika jikoni. Anza kwa kuweka tangawizi na kitunguu saumu. Hakikisha unakaanga kuchelea kuungua. Weka kitunguu maji na endelea kukaanga. Sasa weka nyanya na kisha funika, ili kuruhusu nyanya hizo kuiva kwa mvuke taratibu. Katia hoho na baadaye unga wa binzari nzima, chumvi na pilipili kama utapendelea. Kwa mkate chukua kikombe cha chai. Weka maji nusu na kisha weka hamira chumvi na sukari. Acha viumuke vyenyewe kw