Posts

Showing posts from 2014

Upishi wa tembele la chukuchuku

Image
Mahitaji  Matembele mafungu 2 Nyanya 2 kubwa Kitunguu 1 Chumvi kiasi Mafuta kijiko 1 Ndimu 1 Namna ya kutengeneza Chukua matembele , yachambue na kisha yaoshe. Weka kwenye sufuria ya kupikia. Kata kata nyanya, kitunguu na weka juu yake. Kisha weka chumvi na mafuta na injika jikoni. Weka moto wa kiasi na acha viive kwa muda wa dakika tano. Funua na geuza, vitu vyote vitakuwa vimeiva. Kamulia ndimu na kisha ipua. Matembele yako yatakuwa tayari kwa kuliwa. Waweza kula na ugali ama chakula kingine utakachopendelea.

Afya yako ndio kipaombele chetu

Image
 Fanya mbogamboga na matunda kuwa sehemu ya maisha yako Tumerudi tena. Baada ya kutokuwepo hewani kwa muda , sasa tutakuwa tukikuletea mapishi mbalimbali kama ilivyokuwa awali. Tofauti na kipindi kile, tutakuwa pia tukikuletea dondoo mbalimbali za ulaji mzuri unaozingatia uboreshaji wa afya yako, pamoja na matukio mbalimbali yanayohusiana na mapishi pamoja na chakula kwa ujumla.