Doughnuts
Mahitaji Siagi 1/2 kg Sukari (iliyosagwa) 1/2 kg Mayai 6 Unga 1kg Baking powder 2 teaspoons Kungu manga 1 Namna ya kupika Changanya unga pamoja na kungu manga na baking powder na siagi , Tia yai moja moja hadi uwe donge Kata vidonge vidonge na usukume kama chapatti, kisha kata duara na chukua kifuniko kata katikati ya mduara. Chemsha mafuta jikoni na kisha uchome kiasi kiasi hadi ziishe zote. Vikipata rangi ya udhurungi ipua na nyunyizia sukari, tayari kwa kuliwa