Wali wa Zafarani





Mahitaji
Zafarani ya rangi ya machungwa
Mafuta ya Zeituni vijiko vine vikubwa
Kigunguu kimoja kikubwa kilichokatwakatwa
Pilipili hoho moja iliyokatwa vipande vipande
Kitungu saumu kimoja kikubwa kilichopondwa
Chumvi kiasi
Majani kiasi ya giligilani kwa ajili kupambia 

Jinsi ya kupika
Injika sufuria jikoni na weka mafuta, kitunguu maji na zafarani pamoja na endelea kukaanga pole pole.
Mafuta yatabadilika rangi na kuwa rangi ya machungwa, ipua na weka pembeni kwa muda wa dakika 10. Yachuje na weka kwenye kibakuli
Chukua kijiko kimoja kikubwa cha mafuta na weka katika kikaango. Kisha chukua tena kitunguu maji na kitunguu swaumu endelea kukaanga mpaka vilainike. Kisha ongeza pili pli hoho na endelea kukaanga mpaka iwe laini.
Weka mchele na endelea kukaanga pole pole mpaka mchele utaponukia na kubadilika rangi na kulainika.
Ongeza maji na ufunike iendelee kuiva kwa dakika 8-10 kwa moto mdogo mpaka iive.
Baada ya kuiva kataka majani  giligilani na pamba katika wali wako.
Unaweza kuongeza ladha ya chakula hiki kwa kuweka karanga au zabibu kavu au hata korosho kavu.

Comments

  1. Nimeipenda hii dada, bachelor mimi naenda kurekebisha leo

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu