Tambi za dengu

Mahitaji
Unga wa dengu ½ kilo
Unga wa pilipili binzari nyembamba ½ kijiko cha mezani
Unga wa pilipili manga kijiko 1 cha chai
Unga wa mchele ¼ kilo
Chumvi kiasi
Mafuta ya alizeti ½ lita
Baking powder
Namna ya kutengeneza
Changanya unga wa mchele pamoja na ule wa dengu. Kisha chukua nyunyuzia baking powder na baadaye chumvi. Weka unga wa binzari nyembamba na pilipili manga. Changaya vizuri na kisha weka maji kidogo kidogo huku ukukanda hadi liwe donge gumu kama unavyofanya kwenye maandazi. Baada ya hapo weka donge lako pembeni na funika. Acha likae kwa muda wa nusu saa hadi saa moja.
Baada ya hapo chukua karai la mafuta weka jikoni acha hadi mafuta yapate moto kabisa. Kisha chukua mashine ya kupikia tambi na weka donge lako. Kandamiza taratibu huku ukiruhusu minyororo ya tambi kuingia kwenye mafuta yaliyo jikoni. Weka kiasi kiasi huku ukikaanga. Acha mpaka zitakapokuwa zimeiva na kukauka vizuri. Ipua na weka pembeni. Weka kwenye sahani safi na kavu. Tambi zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Ikiwa huna mashine, unaweza kutumia bakuli ya bati iliyotobolewa mfano wa chujio. Na kisha kandamiza kwenye tundu hizo hadi unga wako upite kwenye tundu za bati hilo na kufanya kama nyuzi nene na ndefu. Fanya kama nilivyoelekeza hapo juu.

Comments

  1. Nashukur kwa maelekezo ntayafanyia kazi maana nilikuwa natamani nijifunze kwa matumiz ya nyumbani

    ReplyDelete
  2. Nashukur kwa maelekezo ntayafanyia kazi maana nilikuwa natamani nijifunze kwa matumiz ya nyumbani

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya