Nyama ya kupaka

1
Mahitaji
Nyama ½ kilo
Mayai 4
Chumvi kiasi
Samli kiasi
Pilipili manga kiasi
Mdaladini, iliki kiasi
Bizari nzima kiasi
Tangawizi iliyosagwa vijiko 2
Limao au ndimu kipande 1
Nyanya nzima za kuiva 4 kubwa
Kitunguuu maji
Pilipili 1 kama unapendelea
Namna ya kuandaa
Chukua nyama na ikatekate vipande vidogo vidogo na kisha ioshe vizuri. Injika jikoni na weka chumvi kiasi, tangawizi na juisi ya ndimu au limao. Changanya na kisha acha ichemke. Baada ya kukauka maji ya kwanza ongeza ya pili ili iive vizuri. Ikishaiva okoa na weka pembeni.
Chukua sufuria nyingine kavu na injika jikoni. Weka samli na kisha anza kwa kukatia katika kitunguu maji na kisha kaanga hadi kiwe cha brown. Weka pilipili manga, iliki, mdalasini na binzari nzima na endelea kukaanga.
Chukua nyanya zako na zikatekate vipande vidogo,vidogo huku ukiendelea kukoroga. Onja chumvi, ikiwa bado haijakolea vizuri, unaweza kuongeza ili iwe na ladha inayokubalika. Funika na cha viive kwa mvuke, kwa muda kama wa dakika tano hivi. Baada ya hapo funua na weka nyama juu yake huku ukiendelea kukoroga.
Zikichanganyika vizuri, pasua mayai yako na weka kwenye bakuli moja. Koroga hadi yachangnyike na kisha, mimina mayai hayo kwenye mchanganyiko wako ulioko jikoni. Koroga kwa muda dakika tatu mpaka nne hivi mchuzi wako utakuwa tayari.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu