Mkate wa ndizi


Mahitaji
Sukari kikombe 1
Siagi 1/3 kikombe
Mayai 2
Ndizi mbivu zilizomenywa na kusagwa kikombe 1 na nusu.
Maji 1/3
Unga wa ngano kikombe 1 na ½ cha chai
Unga wa soda kijiko 1 cha chai
Chumvi kijiko 1 cha chai
Baking poda ¼ kijiko cha chai
Karanga ½ kikombe cha chai
Namna ya kupika
Changanya sukari na siagi kwenye bakuli moja kubwa la udongo ama plastiki. Hakikisha vinachanganyika kabisa. Kisha weka mayai endelea kukoroga. Halafu unga wa ngano. Vikishalainika weka ndizi na saga kwa muda wa dakika tano. Ikiwa unatumia mashine ya kusagia sekunde 30 tu zinatosha kukamilisha zoezi hili.
Chukua viungo vingine vyote vilivyobaki ispokuwa karanga na kisha weka kwenye mchanganyiko wako. Changanya vizuri hadi vichanganyike vizuri.
Acha mchangayiko wako uumuke kwa muda wa dakika 30. Na baada ya hapo mimina katika bati la kuokea taya ri kwa kuoka. Oka kwa muda wa dakika 30 hadi uwe umei va kabisa .
Baada ya hapo opoa na weka pembeni. Acha upoe . Ukishapoa kabisa, katakata silesi .Mkate wako uko tayari kwa kuliwa . Unaweza kula na chai maziwa ama kinywaji chochote kisicho na kilevi.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu