Chips na silesi ya nyama

Mahitaji
Viazi ulaya 1 kilo
Mafuta ya kupikia lita moja
Mayai 4
Nyama isiyo na mfupa silesi 4
Salad kwa ajili ya kupambia
Chumvi , pilipili na ndimu kiasi

Namna ya kuandaa
Chukua viazi menya na katakata katika umbo la chips. Kisha kanga kwenye mafuta hadi vikauke kiasi. Chuja mafuta na kisha weka pembeni.
Chukua silesi za nyama na kisha ipake chumvi na viungo vingine kama utapendelea. Unaweza kukaanga kwenye mafuta ama kuoka kwenye oven. Itakapoiva opoa na weka kwenye shani yenye chips.
Vunja mayai yako na kisha kanga moja moja kwa mtindo wa jicho la ngombe na weka kwenye sahani ya chips.
Gawanja chips zako katika sahani nne na kila moja weka silesi ya nyama na yai lilokaangwa. Baada ya hapo chukua saladi yako na weka pembeni ya kila sahani ya chakula chako hicho.
Chips zako zipo tayari kwa kuliwa. Unaweza kula kwa kinywaji chochote unachopendelea.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu