Supu ya ‘Goulash’


Mahitaji
Nyama isiyo na mifupa ¼ kilo
Tambi ¼ kilo
Karoti kubwa 2
Chumvi kiasi
Pilipili kiasi ikiwa unapendelea
Viazi ulaya ¼ kilo
Vitunguu maji 2 vikubwa
Mafuta ya alisenti vijiko 3 vya mezani
Ndimu 1

Namna ya kutengeneza
Anza na nyama ioshe na kasha ikate vipande vidogovidogo. Kamulia ndimu na injika jikoni. Acha mpaka ive na kasha weka pembeni. Chukua viazi ulaya menya maganda na kasha vikate vipande vidovidogo, weka chumvi. Chemsha hadi viive na kasha wea pembeni. Chukua tambi zivunjevunje. Injika maji jikoni na weka chumvi kiasi pamoja na mafuta. Maji yakichemka weka tambi acha ziive na kisha chuja maji na weka pembeni.
Chukua sufuria kavu na injika jikoni. Miminia mafuta na kisha kaanga vitunguu hadi view vya brown. Katakata karoti vipande vidogo vidogo na kasha weka kwenye sufuria yenye vitunguu. Kanga pamoja. Baada ya hapo weka viazi, nyama na baadaye tambi. Koroga na kasha weka chumvi kiasi na baadaye pilipili.
Koroga koroga ili vichanganyike vizuri, na baadaye weka maji ya kutosha ili kukamilisha upishi wake. Acha ichemke kwa muda na baadaye weka pembeni. Chukua vibakuli vya supu na kasha gawanya supu yako kulingana na kiasi cha walaji ulichokuwa nacho. Supu yako iko tayari kwa kuliwa.
Ikiwa hutapata nyma ya ng’ombe unaweza kutumia aina nyingne ya nyama alimradi isiwe na mifupa. Kwa mujibu wa wapishi mbalimbali, aina hii ya supu ni nzuri zaidi kwa watoto. Hivyo ikiwa utaamua kuwaandalia watoto wako hakikisha huweki pilipili.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu