Chauro

Mahitaji
Pepeta 1/4kg
Karanga 1/4kg
Viazi ulaya 1/4kg
Dengu 1/4kg
Chumvi kijiko cha chakula
Sukari kijiko cha chakula
Pilipili ya unga kijiko cha chakula
Mafuta ya kula lita moja

Namna ya kutengeneza
Menya viazi vioshe na vikatekate slesi. Weka karai la mafuta jikoni. Baada ya kuchemka weka viazi na vikaange hadi viive na kukauka. Osha karanga na kisha zikaange hadi zikauke. Osha dengu nazo zikaange. Baada ya hapo ukivitoa kwenye mafuta. Vichuje na kisha ziweke hadi zipoe.
Vikishapoa vichanganye. Kisha weka kikavu na chenye nafasi. Nyunyizia sukari kiasi chumvi na pilipili.
Chauro zako tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu