Keki ya jam


Maandalizi dakika 15 upishi dakika 25

Mahitaji
Unga wa ngano ¼ kilo
Sukari ya kawaida ¼ kilo
Siagi ¼ kilo
Mayai 6
Arki (Vanilla) matone matatu
Baking powder kiasi
Unga wa kakao kiasi ( kama utapendelea)

Vya kupambia

Jam ya mchanganyiko wa matunda kikombe kimoja cha chai
Zabibu kavu nusu kikombe cha chai
Apple moja kubwa
Sukari laini (icing sugar)

Namna ya kuandaa

Kwenye bakuli kubwa ya udongo, weka siagi na baking powder, sukari na kisha changanya taratibu. Halafu pasua mayai yote na kisha endelea kukoroga. Baada ya hapo weka unga na changanya hadi uwe uji mzito. Chukua arki na nyunyizia kwenye mchanganyiko wako. Hii itasaidia kuifanya keki yako iwe na harufu nzuri.
Ikiwa utapendelea keki yako kuwa na rangi ya brown si vibaya ukachanganya na unga wa kakao

Kwenye bakuli nyingine pembeni. Chukua jam changanya na zabibu kav
u. Chukua apple na menye maganda yake na katakata silesi. Kisha weka kwenye mchanganyiko wako huo.

Chukua bati la kuchomea weka uji wako wa keki nusu . Juu yake weka mchanganyiko wote wa jam. Baadaye miminia uji uliobaki juu yake. Oka kwa muda wa dakika 20 hadi 25 kwa moto wa kiasi.

Baada ya keki kuiva, opoa na weka pembeni na kisha nyunyizia icing sugar kwa juu.

Keki hii inaweza kuliwa na watu nane kama desert baada yamlo.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu