Supu ya samaki mchangayiko


Mahitaji
Minofu ya ndualo, ngizi na kamba wakubwa kilo 1
Chaza ¼ kilo
Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya chakula
Vitunguu maji vikubwa viwili vilivyokatwakatwa
Vitungu saumu punje nne vilivyosagwa
Vijiti vya figili viwili vilivyokatwakatwa vipende vidogovidogo
Viazi ulaya vitatu vilivyokatwakatwa vipande vodogovidogo.
Nyanya zilizomenywa na kukatwakatwa vipande vidogovidogo 1/4 kilo
Nyanya ya kopo kijiko kimoja
Majani ya giligilani fungu 2
Maganda ya machungwa 2
Limao au ndimu 1
Chumvi kiasi
Pilipili kiasi
Mvinyo mweupe kifuniko 1 cha chupa yake

Namna ya kutengeneza

Chukua samaki wako osha vizuri na kisha katakata vipande vidogovidogo kiasi hakikisha haviwi vidogo sana. Kwa upande wa kamba ondoa magamba yake kwanza kabla ya kuwaosha . Kisha weka pembeni kwenye bakuli safi na kavu.
Kwa upande wa chaza waweke jikoni peke yake kwanza kisha chukua mvinyo miminia . maji yakiaza kupata moto , wote watajifungua. Na  ndipo uwaoshe vizuri na kisha changanya na mchanganyiko wako wa samaki bila kuwatoa magamba yake.
Chukua sufuria na kisha injika jikoni halafu weka mafuta ya mzeituni. Weka vitunguu maji na saumu na kisha kaanga hadi vilainike.Weka figili  viazi na majani ya giligilani fungu moja, yaliyokatwakatwa, huku ukiendela kukaanga kwa dakika mbili hivi.Weka nyanya na maganda ya chungwa na pika kwa muda wa dakika tano. Kisha ondoa maganda hayo.
Weka mchanganyiko wako wa samaki acha uchemke kwa muda ikiwa maji ya nyanya yatakauka, ongeza maji kidogo kidogo hadi samaki wako watakapokuwa wameiva. Baada ya hapo weka kiasi cha supu cha kukukidhi mahitaji ya watu wanne.
Mimina kwenye bakuli za supu. Katia katia lile fungu moja la giligiliani juu ya kila bakuli. Ikiwa utapendelea kutumia ndimu huo ndio muda wake, Unaweza kuongeza ndimu na viungo vingine kama pilipili.Supu yako ipo tayari kwa kuliwa. Unaweza kula kwa mkate ama kitafunwa chochote utakachopendelea, ingawaje si vibaya pia ikiwa utakula peke yake.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu