Chatini ya karoti ,nazi na kitunguu


Mahitaji
Kitunguu kimoja kikubwa
Karoti moja kubwa
Nazi iliyokunwa nusu kikombe
Pilipili mbuzi moja au mbili
Kotmil fungu moja
Rojo ya ukwaji nusu kikombe cha chai
Chumvi kiasi

Namna ya kutengeneza
Kabla ya kuanza utengenezaji wakom hakikisha mbogamboga zako zinaoshwa kwa maji ya moto ili kuziweka katika hali ya usalama zaidi kiafya.
Baada ya hapo, chukua karoti na vitunguu maji, katakata katika vipande vidogovidogo, kisha weka kwenye bakuli, chukua viungo vingine vyote changanya kwenye mchangayiko huo.
Baada ya hapo weka kwenye mashine ya kusagia matunda, weka maji kiasi ili kurahisisha usagaji wake. Saga hadi vilainike kabisa na kuwa uji mzito, ondoa kwenye mashine na mimina kwenye bakuli tayari kwa kuliwa.

Kama nilivyokueleza hapo juu, kuwa unaweza kula na chakula chochote unachopendelea kulingana na mahitaji yako.

Ikiwa utapendelea kuwapa watoto, unashauriwa kutoweka pilipili wakati wa maandalizi yake.

Chatini ya nazi mara nyingi hupendeza sana ikiwa italiwa ‘fresh’. Hivyo unashauriwa kutengeneza kiasi cha matumizi yako, ili kuepuka kuilaza, kwani ikiwa italala na ikaliwa, mlaji hatapata ladha yake halisi.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu