Halua ya boga


Mahitaji
Boga ½ kilo
Sukari ½ kilo
Samli ½ Kilo
Unga wa hiliki ½ kijiko cha chai
Namna ya kutengeneza
Chukua boga lako menya na kisha katakata vipande vidogo vidogo na kisha chemsha hadi viive na kuwa laini kabisa.
Baada ya kuvia mwaga maji na saga mpaka uwe laini. Chukua sukari na samli na kisha changanya kwenye boga lako. Injika jikoni huku ukiendelea kusonga taratibu hadi viive vizuri.
Tumia moto mdogomdogo ili kuepuka kuungua. Acha iendelee kuiva kwa muda dakika kumi na kisha ipua. Chukua sahani ya bati na ioshe na maji kisha mwaga bila kufuta. Mimina sahanini na kisha tandaza.
Acha hadi ipoe. Unaweza kula na kahawa uji n.k

Si hivyo unaweza kula kama ‘desert’ mara baada ya kupata mlo kamili.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu