Saladi ya nyama

Mahitaji
Nyama ½ kilogram
Mafuta 1/3 kikombe
Juisi ya limao vijiko 2
Kitunguu saumu kilichopondwa vijiko 2
Chumvi ½ kijiko cha chai
Pilipili manga ½ kijiko cha chai
Nyanya 2 zilizoiva
Karoti 1
Pilipili hoho 1
Majani ya saladi kiasi
Tangawizi iliyopodwa kijiko 1
Namna ya kuandaa
Anza kwa kuosha vizuri nyama. Kisha paka tangawizi, chumvi na vitunguu saumu kwenye nyama hiyo. Kisha nyunyizia unga wa pilipili manga.
Ikiwa unatumia jiko la ‘oven’. Anza kwa kupaka mafuta kwenye waya wa kuchomea. Na kisha weka nyama kwenye oven. Ikiwa unatumia jiko la kawaida fanya hivyo hivyo ili kuchelea kuganda kwa nyama wakati wa kuchoma.
Tandaza nyama yako vizuri kwenye waya wa kuchomea na kisha acha hadi iive. Hakikisha unaigeuzageuza ili kuepuka kuungua.
Wakati nyama ikiwa jikoni, andaa saladi yako taratibu kwa kuosha vizuri na kukatakata vipande vidogo vidogo. Panga vizuri katika sahani yako tayati kwa kuliwa.
Weka kwa mpangilia mbogamboga zako, hii itakusaidia kuifanya saladi yako iwe kama ua. Hakikisha unapanga vizuri nyanya na hayo majani ya kijani.
Angalia kwa makini nyama yako ikiwezekana onja kuona kama imeiva. Kisha katia katia vipande vya nyama katika saladi.
Saladi ya nyama huweza kuliwa wakati wowote.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu