Pilau ya zabibu

Mahitaji
Mchele kilo 1 Kuku ½ kilo Kitunguu maji 1 chenye ukubwa wa wastani Mafuta ya kupikia ¼ lita Kitunguu saumu 1 kikubwa Tangawizi mbichi 1
Mdalasini nzima vijiko 2 Iliki vijiko 2 vya mezani Uzile/ binzari nyembamba vijiko 2 vya mezani
Zabibu kavu ½ kikombe cha chai.
Namna ya kupika Mkate kuku au nyama na muoshe kisha mweke katika sufuria kisha weka chumvi na uchemshe mpaka awive kisha epua. Menya kitunguu maji na saumu kisha vitwange hadi vilainike.
Chukua mdalasini, iliki na bizari utwange pamoja kisha uchunge unga laini saga thomu na tangawizi mbichi. Weka jikoni sufuria tia mafuta kisha anza kwa kukaanga kitunguu maji hadi kiwe na rangi ya hudhurungi kisha weka saumu kaanga kwa muda kisha tia viungo vilivyosalia.
Tia vipande vya kuku halafu supu iliyosalia katika sufuria acha ichemke na vitu vyote mpaka ibaki rojo rojo. Wali ukisha upakue, utavimwagia juu ya wali ukipenda utapambia zabibu juu yake. Zabibu hizo ziloweke kwanza.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu