Saladi ya kuoka ya mbogamboga


Mahitaji

Pilipili hoho nyekundu 2
Mafuta ya parachichi au lozi (olive)vijiko 3 vya chai
Mvinyo mwekundu kijiko 1 cha chai
Kitunguu saumu punje 3 zilizosagwa
Pilipili mbuzi moja iliyokatwakatwa
Biringanya 1, lilokatwa silesi
Kitunguu maji 2 vilivyokatwa silesi
Nyanya 6 zilizokaushwa kwa jua
Majani ya bazili kiasi
Vinega kiasi
Lozi nzima (olive) kiasi

Namna ya kutengeneza

Chukua bati la kuokea, katakata hoho katiak vipande vidogovidogo na kasha weka ndani yake. Oka kwa dakika 15 hadi zilegee. Ondoa na weka pembeni. Wakati zinapoa, changanya mafuta, kitunguu saumu na pilipili mbuzi.

Weka kwenye bati la kuokea pamoja na silesi za biringanya na vitunguu weka chumvi kidogo kisha oka kwa moto wa kiasi. Acha hadi vilainike kiasi.

Kwenye bakuli nyingine changanya , hoho, nyanya, lozi nzima kiasi na majani ya bazili. Kisha changanya pamoja na mbogamboga zako ulizooka.

Saladi yako ipo tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu