Mapishi ya tambi

Futari za tambi

Mahitaji

Tambi ½ kg
Maziwa 1/2lita
Sukari kiasi
Chumvi
Maji 1lita
Vanilla au unga wa hiliki ½ kijiko cha chai.
Namna ya kupika
Chukua maji na kisha weka chumvi kiasi cha nusu kijiko cha chai, injika maji jikoni na kisha yaache yachemke, weka tambi zako katika maji hayo acha zichemke kwa muda wa dakika tano.
Baada ya hapo chukua hizo tambi na ziche maji yote na kisha miminia maziwa, weka sukari kiasi unachohitaji na mwisho weka vanilla au hiliki na kisha funika.
Acha vichemke hadi maji yatakapoisha, pakua tayari kwa kuliwa.

Tambi za kupalia

Mahitaji
Tambi ½ kg
Maji lita 1
Chumvi kiasi
Tui bubu la nazi kikombe 1 cha chai
Sukari kiasi
Namna ya kupika
Chukua maji yaweke jikoni na kisha weka chumvi 1/2 kijiko cha chai, acha maji yachemke na kisha weka tambi acha zichemke kwa muda wa dakikia tano zitakuwa zinakaribia kuiva. Baada ya kuhakikisha kuwa zinakaribia kuiva zichuje maji yote na kisha weka tui la nazi sukari na unga wa hiliki.
Acha maji yakauke kabisa na kisha palia mkaa au weka kwenye oven kama unavyofanya kwa wali.
Baada ya dakika kumi tambi zako zitakuwa ziko tayari kwa kuliwa.
Futari hizi kwa kawaida huliwa kwa na uji au chai

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu