Sambusa za mbogamboga


Mahitaji
Unga wa ngano ½
Viazi ulaya ¼kg
Maji ya uvuguvugu kiasi
Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 kikubwa
Tangawizi kiasi
Pilipili mbuzi 1 (kama unatumia)
Vitunguu Maji 3
Viungo kiasi
Chumvi kiasi
Njegere mbichi kikombe 1
Chumvi kiasi


Unga wa ngano vijiko 3 vya chakula.

Namna ya kutengeza

Chukua unga wa ngano ½ kg na kanda hadi ulainike kama unavyofanya kwa unga wa maandazi.
Baada ya hapo chukua mbogamboga zote katakata vipande vidogovidogo na kisha waka chumvi na baadaye viungo vya unga,kisha weka jikoni.
Baaada ya dakika tano ipua na weka chini.

Gawa unga ukioukanda katika sehemu kumi. Tandaza kidogona kisha paka mafuta juu yake. Sukuma kama chapatti na kisha weka kwenye chuma cha kukaangia chapatti bila ya kuweka mafuta.
Baada ya kubabua weka kwenye kibao cha chapati na kicha kwenye kibao halafu kata sehemu nne.

Chukua unga wa ngano vijiko 3 vya mezani na kisha tengeneza uji mzito kwa ajili ya kugandisha sambusa zako.
Tengeneza umbo la koni kutoka kila kipande cha chapatti ulichokata. Jaza mchanganyiko wa mbogamboga ndani yake. Funga sehemu ya juu funga sehemu zote kwa kugandisha na uji uliotengeneza.

Fanya hivyo hadi chapatti zote ziishe. Chukua mafuta na weka jikoni, yakipata moto weka sambusa zako. Kaanga hadi ziwe rangi ya hudhurungi.


Ipua na chuja mafuta katika chujio la bati. Baada ya hapo sambusa zako zitakuwa tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu