Wali wa rangi tatu

Mahitaji
Kwa wali wa njano
Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai
Mafuta ya kupikia kijiko1 ½
Nyanya 2 zilizomenywa na kukatwakatwa
Karoti 3 zilizochemshwa na kuiva
Unga wa binzari 1/4 kijiko
Chumvi kiasi
Kwa wali wa mweupe
Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai
Mafuta ya kupikia kijiko1 ½
Tui la nazi kikombe 1
Unga wa hiliki Kijiko 11/2 chachai
Kwa wali wa kijani
Mchele wa basmati kikombe 1 cha chai
Mafuta ya kupikia kijiko 1 ½
Chumvi kiasi
Vitunguu maji 2
Kitunguu saumu kilichopondwa 1
Tangawizi iliyopondwa 1
Nazi iliyosagwa vijiko 2
Majani 8 hadi 10 ya mnanaa
Majani ya giligilani kikombe kimoja
Pilipili manga kijiko 1
Garam masala kijiko 1 cha chai
Namna ya kuandaa
Unatakiwa kupika wali walo katika sufuria tatu tofauti. Kwa wali mweupe unatakiwa kupika kama ilivyozoeleka huku ukiongeza hiliki kama kiungo chako.
Unachotakiwa kufanya ni kuosha mchele wako. Kisha injika tui jikoni weka chumvi na baadaye hiliki. Hakikisha maji uliyoinjika yana uwezo wa kuivisha wali wako. Baada ya kuiva palia na weka pembeni.
Kwa wali wa rangi ya machungwa
Anza kwa kupika wali wa mafuta. Kwa kuosha mchele na kuuchemsha kwa kiwango cha maji ya kutosha kuivisha. Hakikisha unaweka chumvi ili kuufanya wali wako kuwa na ladha.
Chukua karoti na nyanya saga pamoja. Kisha kaanga binzari na changanya na mchanganyiko wa nyanya na karoti. Chukua wali wako uliokwishawiva na changanya katika mchanganyiko wako huo. Wali wote utakuwa wa rangi ya chungwa.
Kwa wali wa kijani , anza kwa kupika wali wenyewe kama nilivyoelekeza hapo juu.Kisha chukua kitunguu maji, saumu, tangawizi nazi , majani ya mnanaa,majani ya giligilani,hoho, pilipili manga na kisha saga kwenye machine ya kusagia.
Chukua mafuta ya kupikia weka jikoni, na kaanga garam masala na baadaye weka mchangayiko wako wa kijani kwenye sufuria hiyo iliyoko jikoni. Endelea kukaanga hadi viive kabisa. Ipua na changanya na wali wako. Utapata wali wa kijani.
Baada ya hapo pakua. Na weka kwenye bakuli lenye muundo unaopendelea. Anza kwa kuweka rangi yeyote kati ya hizo ulizopika. Panga vizuri kwa kufuata mpangilio maalum unaweza kuanza na rangi ya machungwa, nyeupe na kijani ikaja mwisho au kinyume chake.
Pamba wali wako kwa kuweka jani dogo la giligilani na kipande cha karoti.
Chakula choko kipo tayari kwa kuliwa

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu