Mahitaji
Unga wa ngano wa Atta nusu kilo
Mtindi robo lita
Maji ya vuguvugu kiasi cha kukandia
Hamira kijiko kimoja cha chai
Chumvi kiasi kama utapendelea
Trei za kuokea mikate
Namna ya kuandaa
Chukua bakula kavu na kubwa kiasi  la kukandia unga wako. Weka unga, chumvi na kisha hamira.
Changanya mchanganyiko wako huo kabla ya kutia majimaji . kisha weka maziwa ya mtindi endelea kuchanganya hadi ukandike. Kama una maziwa ya mtindi ya kutosha, unaweza kukanda kwa kutumia maziwa hayo pekee hadei unga wako ulainike kabisa. Wakati ukiendelea kukanda kama utaona kuna haja ya kuongeza maji waweza ongeza yale ya uvuguvugu.
Ukishalainika acha uumuke inaweza kuwa kwa muda wa dakika 20 hadi 30, hii itategemea na ukali wa hamira uliyotumia.
Ukishaumuka, chukua na ukande tena baada ya hapo kata na weka kwenye trei za kuokea mkate. Funika na acha kwa muda wa dakika tano hadi sita . Kisha anza kuoka kwa moto wa kiasi. Hakikisha unaiva na kuwa wa rangi ya hudhurungi. Mkate wako uko tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu