Jeli ya embe na nazi

Mahitaji
 Jeli ya embe Embe lililoiva lisilo na nyuzinyuzi moja
 Juisi ya embe kikombe 1 cha chai
Gelatin kijiko kimoja cha chakula
Sukari vijiko vitatu vya chakula
Juisi ya ndimu kijiko kimoja cha chai
Maji nusu kikombe cha chai

 Jeli ya tui la nazi 
 Tui la nazi kikombe kimoja cha chai
Sukari vijiko viwili
Chumvi kiasi
Gelatin kijiko kimoja cha chakula

 Namna ya kutengeneza
 Chukua sufuria kavu na weka jikoni. Miminia juisi ya embe na kisha weka sukari na koroga kisha weka gelatin. Endelea kukoroga had I vichanganyike.Baada ya kuchemka kwa dakika Tano hadi kumi utakuwa umebaki urojo unaotosha kutengeneza jelly. Ipua na weka chini kisha tia juisi ya ndimu na lile embe ulilonalo likate vipande vidogovidogo na weka kwenye uji wako huo. Koroga na kisha mimina kwenye bakuli kavu la kioo lenye nafasi kiasi. Baada ya hapo chukua tui la Nazi na injika jikoni na kisha miminia sukari na gelatin pamoja na chumvi kiasi. Koroga na viache vichemke hadi vitengeneze uji. Kisha mimina kwenye bakuli lenye ule uji wa embe. Acha vikauke kwa muda wa dakika Tano. Katakata katika vipande vidogo vidogo tayari kwa kuliwa. Aina hii ya Jelly inaweza kuliwa kama kitindamlo.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu