Wali wa Zafarani
Mahitaji
Zafarani ya rangi ya machungwa
Mafuta ya Zeituni vijiko vine vikubwa
Kigunguu
kimoja kikubwa kilichokatwakatwa
Pilipili
hoho moja iliyokatwa vipande vipande
Kitungu
saumu kimoja kikubwa kilichopondwa
Chumvi
kiasi
Majani
kiasi ya giligilani kwa ajili kupambia
Jinsi ya kupika
Injika sufuria jikoni na weka mafuta, kitunguu maji na
zafarani pamoja na endelea kukaanga pole pole.
Mafuta
yatabadilika rangi na kuwa rangi ya machungwa, ipua na weka pembeni kwa muda wa
dakika 10. Yachuje na weka kwenye kibakuli
Chukua
kijiko kimoja kikubwa cha mafuta na weka katika kikaango. Kisha chukua tena
kitunguu maji na kitunguu swaumu endelea kukaanga mpaka vilainike. Kisha ongeza
pili pli hoho na endelea kukaanga mpaka iwe laini.
Weka
mchele na endelea kukaanga pole pole mpaka mchele utaponukia na kubadilika
rangi na kulainika.
Ongeza
maji na ufunike iendelee kuiva kwa dakika 8-10 kwa moto mdogo mpaka iive.
Baada
ya kuiva kataka majani giligilani na
pamba katika wali wako.
Unaweza
kuongeza ladha ya chakula hiki kwa kuweka karanga au zabibu kavu au hata
korosho kavu.
Nimeipenda hii dada, bachelor mimi naenda kurekebisha leo
ReplyDelete