Mkate wa mbogamboga

Mahitaji
Mbogamboga za kujazia
Vitunguu vitatu vilivyokatwakatwa
Nyanya 2 zilizokatwakatwa
Hoho 1 ilikatwakatwa
kitunguu saumu kilichopondwa kijiko 1 cha mezani
Tangawizi iliyosagwa kijiko 1 cha mezani
Unga wa bizari nzima kijiko 1 cha chai
Sukari kijiko 1 cha chai
Kotmiri fungu 1
Mafuta ya kupikia kiasi
Chumvi kiasi

Kwa mkate
unga wa ngano vikombe 3 vya chai
Hamiara kijiko 1 cha chakula
Suakri kijiko 1 cha chakula
Chumvi kijiko 1 cha chai
Mafuta ya kula vijiko 2
Jibini kiasi

Namna ya kuandaa
Vya kujazia
Chukua mafuta na weka kwenye sufuria kisha ijika jikoni. Anza kwa kuweka tangawizi na kitunguu saumu. Hakikisha unakaanga kuchelea kuungua. Weka kitunguu maji na endelea kukaanga.
Sasa weka nyanya na kisha funika, ili kuruhusu nyanya hizo kuiva kwa mvuke taratibu.
Katia hoho na baadaye unga wa binzari nzima, chumvi na pilipili kama utapendelea.

Kwa mkate

chukua kikombe cha chai. Weka maji nusu na kisha weka hamira chumvi na sukari.
Acha viumuke vyenyewe kwanza ili kurahisisha uumukaji wa unga wako. Baada ya hapo chukua bakuli yenye nafasi. Weka unga wako na kisha nyunyizia mafuta ya kupikia. Changanya vizuri na baadaye weka mchangayiko wako wa hamira.
Changanya na endelea kuweka maji kidogokidogo huku ukiendelea kukanda hadi liwe donge gumu.
Baadaya ya hapo chukua donge hilo na ligawanye katika matonge mengine madogomadogo manne.
Tandaza katika kibao cha kusukumia chapati kama unavyofanya kwenye chapati. chota mchanganyiko wako na kisha weka katikati ya chapati hiyo. chukua jibini yako na kwaruza ili kupata unga wake. Weka juu ya huo mchangyiko wa mbogamboga. Kunja vizuri na kisha weka pembeni. Fanya hivyo kwa madonge yote na kisha acha kwa muda wa dakika 15 hadi 30. Utakuwa umeumuka vizuri.

Baada ya hapo weka kwenye bati la kuokea ama sufuria. Oka. Hakikisha mikate hiyo inaiva na kuwa na rangi ya hudhurungi.
Mkate wako uko tayari kwa kuliwa. Katika kipindi hiki cha mwezi wa ramadhani unaweza ukatumia kama daku ama futari.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu