Visheti vya kilua


Mahitaji 

Unga wa ngano 1kg
Sukari 1/4 kg
Nazi iliyokunwa kikombe 1 cha chai
Samli 1/4 kg
Vanilla matone matatu
Icing Sugar 1/2kg
Mafuta ya kula 1/2 Lita
Baking powder kijiko 1 cha chai
Maji vikombe 2 vya chai


Namna ya kutengeneza 
Changanya samli na Nazi . Baada ya hapo weka baking powder endelea kuchanganya na kisha weka unga na vanilla. Changanya hadi vichanganuike vizuri. Weka maji kidogo kidogo hadi update donge gumu. Kata matonge Mdogo Mdogo tayari kwa kusukuma. Sukuma taratibu na kisha kata mkato wa kashata
Baada ya hapo kuñja kwa kukutanisha na kubinua pembe ili upate umbo la kilua.
Ukimaliza injika karai la mafuta jikoni na anza kukaanga. Hakikisha haviwi brown sana lakini vinaiva na kukauka.Chukua icing sugar weka kwenye bakuli pana na kisha baada ya kuopoa visheti vyako chuja mafuta na weka kwenye bakuli hilo lenye sukari. Peta ili kuruhususukari ichanganyike vizuri. Hakikisha unafanya hivyo vikiwa bado vya moto.Fanya hivyo kwa vipande vyote. India kwenye bakuli la sukari na weka kwenye sahani tayari kwa kuliwa.

Comments

Popular posts from this blog

Upishi wa tembele la chukuchuku

Tambi za nyanya

Tambi za dengu